2010
Hakuna aliye Kamili
Machi 2010


Vijana

Hakuna aliye Kamili

Mimi siku zote nimetamani kuwa kama Nefi: mtiifu wa dhati, muaminifu mkuu,na mwenye roho ya kina. Katika macho yangu Nefi alikuwa mfano mkuu wa wema. Vitu vichache vinanipendeza mimi zaidi ya dhana ya kukua na kuwa kama yeye—au angalau kuanza kuwa na hata sehemu ya ubora wake.

Siku moja nilikuwa na matatizo madogo, yaliyoletwa na hisia za kutojitosheleza. Nilikuwa na tamaa kuu na malengo mengi. Lakini nilikuwa nikioenekana kutopata mafanikio yoyote. Nikiwa na Majozi ya kukata tamaa, nilielezea hisia hizi kwa baba yangu. Mara moja alisimama, na kutembea hadi kwenye kasha la vitabu, na akatoa mojawapo ya nakala zake za Kitabu cha Mormoni. Bila kusema neno, aliifungua kwenye 2 Nefi 4 na akaanza kusoma mstari wa 17.

Mzizimo ulizangaa kwenye mwili wangu wote kama umeme nilipokuwa nikisikiliza maneno haya ya nguvu: “Ewe mimi mtu mwovu” Fikira zangu zilikimbia. Nefi, shujaa wangu na mfano, angelisema vipi kwamba alikuwa “mtu mwovu”? Kama alikuwa mtu mwovu, hicho kilifanya mimi kuwa nani?

Tena, umeme ulivuma ndani yangu baba yangu alipokuwa akisoma mstari 28: “Amka,roho yangu! Usilemewe na dhambi.” Nilisikia kama vile wingu la giza katika akili yangu lilitawanywa na kuondolewa ili kufunua shauku na wangavu wa wingu wazi la bluu na jua angavu. Sio rahisi kuelezea vile huu mstari uliangaza nafsi yangu. Mistari michache ya maandiko yamenijaza tumaini, maongozi, na furaha kama hii ilivyofanya.

Katika mstari wa 30, Nefi alisema hasa kile nilichokuwa nikifikiria, tu katika maneno ya umbuji mwingi: “Nafsi yangu itashangilia kwaajili yako, Mungu wangu, na mwamba wa wokovu wangu.” Mstari huu ulileta hisia ya amani na shukrani kwa nehema nyororo za Bwana na upendo.

Baba yangu alifunga kitabu na kuelezea kwamba mistari hii mara nyingine uitwa zaburi ya Nefi. Alafu alinifunza kwa makini kwamba hata watu wakuu katika dunia sio kamili, na watu hawa sharti watambue ukosefu wao au kwa vingine watakuwa na kiburi na, kwa hivyo, wasiwe wakuu.

Nilifahamu. Kwa sababu tu nilikuwa na unyonge haikumaanisha nilikuwa siwezi kuwa kama Nefi. Kutambua unyonge wangu ulinileta karibu na hadhi ya Nefi. Nefi alikuwa mkuu kwa sababu, vile vile akiwa mtiifu na mwaminifu, alikuwa mnyenyekevu na tayari kukubali makosa yake.

Tangu uzoefu huu, nimeyathamini sana maneno haya ya Nefi. Kila wakati ninapoyasoma, napata muemuko huo huo na maangozi kama yale ya kwanza nilipoyasoma. Mistari hii inaniimbia kwamba mimi ni binti wa Mungu, mwenye uwezo mkuu zaidi ya vile ningeweza kudhania. Najua kwamba kama nitakuwa mwaminifu na kusonga mbele, baraka zisizoweza kusemeka zimehifadhiwa.