Ujumbe wa Urais wa Kwanza, Machi 2010
Ujasiri wa Kimaadili
Mojawapo ya madhumuni ya maisha ya duniani ni kumuonyesha Mungu kwamba tutatii amri Zake ilihari hii huitaji ujasiri. Tulipita mutihani huo katika ulimwengu wa kiroho. Lakini thuluthi moja ya majeshi ya mbinguni yaliasi dhidi ya pendekezo kwamba watajaribiwa katika kuishi kimwili ambapo palikuwepo na hatari kwamba wangeweza kuanguka.
Kabla hatujazaliwa, tulimjua Mungu Baba na Mwanawe, Yesu Kristo, kibinafsi. Tungeweza kuwaona Wao na kuwasikiliza Wao jinsi walivotufunza na kutuhimiza sisi. Sasa pazia imewekwa juu ya akili zetu na kumbukumbu zetu. Shetani, baba wa uwongo, anajinufaisha kwa sababu ni lazima tuone uhasili wa kujua sisi ni kina nani kupitia macho ya imani, ilihali miili yetu inatufanya kuwa chini ya majaribio na udhaifu wa kimwili.
Tuna usaidizi mkuu wa kutupatia ujasiri katika maisha haya. Mkuu ni Upatanisho wa Yesu Kristo. Kwa sababu ya kile alichofanya, dhambi zinaweza kuoshwa katika maji ya ubatizo. Tunaweza kufanya upya hio baraka wakati tunashiriki katika sakramenti kwa imani na kwa moyo wa toba.
Vipawa vya Kiroho ni usaidizi mwengine Tunapokea Roho wa Kristo wakati wa Kuzaliwa. Hiyo inatupatia uwezo wa kujua wakati uchaguzi ulio mbele yetu utatuelekeza kwenye maisha ya milele. Maandiko ni kielelezo cha kweli tunapoyasoma pamoja na Roho Mtakatifu kama mwenzi wetu.
Roho Mtakatifu utuacha tukaonyesha shukrani na kuuliza usaidizi katika maombi kwa uwazi na uhakika tuliofurahia tulipokuwa na Baba wetu wa Mbinguni na ambao tutakuwa nao tutakaporudi Kwake. Kwamba mawasiliano na Mungu yanasaidia kuondoa hofu kutoka katika mioyo yetu yanajenga imani na upendo wa Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo.
Ukuhani mtakatifu unatupatia sisi ujasiri katika huduma yetu. Katika ibada zake tunapokea uwezo wa kuwatumikia watoto wa Mungu na kustahimili mvuto wa uovu. Anapotuita sisi kuhudumu, tuna ahadi hii: “Na yeyote awapokeaye, hapo nitakuwepo pia, kwani nitakwenda mbele ya nyuzo zenu. Nitakuwa mkononi mwenu wa kulia na wa kushoto, na Roho wangu atakuwa mioyoni mwenu, na malaika wangu watawazingira, ili kuwabeba juu (M&M 84:88).
Nabii Joseph Smith katika huduma yake alikuwa na sababu ya kuwa na hofu. Lakini Mungu alimpatia ujasiri kwa uhakikisho huu wa mfano wa Bwana:
”Kwa maana utatupwa ndani ya shimo, au katika mikono ya wauaji, na hukumu ya kifo ikapitishwa juu yako; kama utatupwa kilindini; kama mawimbi makali yatakula njama dhidi yako; kama upepo mkali utakuja kuwa adui yako; kama mbingu zitakusanya giza, na vitu vyote vya asili vikiungana ili kuzingira njia yako; na juu ya yote, kama mataja yale ya jahanamu yataachana kinywa wazi kwa ajili yako, fahamu wewe, mwanangu, kwamba mambo haya yote yatakupa wewe uzoefu, na yatakuwa kwa faida yako.
”Mwana wa Mtu ameshuka chini yao wote. Je, wewe u mkuu kuliko yeye? (M&M 122:7–8)
Mungu ametupatia sisi usaidizi wa kupindukia wa kuondoa hofu na kutupatia ujasiri, katika chochote tutakachokabiliana nacho. Tunapotafuta usaidizi Wake, Anaweza kutuinua kuelekea ule uzima wa milele tunaotafuta.