2010
Kuimarisha Imani katika Mungu Baba na Yesu Kristo kupitia Masomo ya Maandiko ya Kibinafsi
Machi 2010


Ujumbe wa Mwalimu Mtembelezi, Machi 2010

Kuimarisha Imani katika Mungu Baba na Yesu Kristo kupitia Masomo ya Maandiko ya Kibinafsi

Funza maandiko na dondoo hizi, au, ikihitajika, kanuni nyingine ambayo itabariki akina dada unaowatembelea. Toa ushuhuda wa fundisho hili. Alika wale unaowafundisha kushirikisha walichohisi na kujifundisha.

”Nilipokuwa bibi arusi mpya, … nilialikwa kwa mlo wa chakula cha mchana wa kina dada wote wa Muungano wa Usaidizi wa Akina Mama katika kata yangu ambao walikuwa wamesoma kati ya Kitabu cha Mormoni au kitabu kifupi cha historia ya Kanisa. Nilikuwa mzembe katika kusoma maandiko, kwa hivyo nilihitimu kuudhuria chakula cha mchana kwa kusoma kitabu kifupi kwa sababu kilikuwa rahisi na kilichukua muda mfupi. Nilipokuwa nikila chakula changu cha mchana, nilikuwa na hisia nzito kwamba hata kama kitabu cha historia kilikuwa kizuri, ningesoma Kitabu cha Mormoni. Roho Mtakatifu alikuwa ananishawishi kubadilisha tabia yangu ya kusoma maandiko Siku hiyo hiyo nilianza kusoma Kitabu cha Mormoni, na sijawahi kusimama kamwe. … Kwa sababu nilianza kusoma maandiko kila siku, nimejifunza juu ya Baba wangu wa Mbinguni, Mwanawe Yesu Kristo, na kile ninachohitaji kufanya ili kuwa kama Wao. …

Kila mwanamke anaweza kuwa mwalimu wa injili nyumbani mwake, na kila mwanadada Kanisani anahitaji elimu ya injili kama kiongozi na mwalimu. Kama bado hujaanza tabia ya kusoma maandiko kila siku, anza sasa na uendelee kujifunza ili kujitayarisha kwa majukumu yako katika maisha haya na katika milele.”1

Julie B. Beck, Rais mkuu wa Muungano wa Usaidizi wa Akina mama.

”Kujifunza kwa maandiko kutasaidia ushuhuda wetu na ushuhuda wa wanafamilia wetu. Watoto wetu leo wanakua wakizingirwa na sauti zinazowashawishi kuachilia kile kilicho sawa na kufuata, badala yake, anasa za ulimwengu. Wasipokuwa na msingi imara katika injili ya Yesu Kristo, ushuhuda wa kweli, na azimio la kuishi vyema, watakuwa wanaweza kuathirika na mvuto huu. Ni jukumu letu kuwalinda na kuwakinga.”2

Rais Thomas S. Monson.

”Tunataka kina dada zwtu wawe wasomi wa maandiko. …Mnahitaji uzoefu na ukweli wake wa milele, kwa ufanisi wako mwenyewe, na kwa madhumuni ya kuwafundisha watoto wenu wenyewe na wale wengine wanaokuja katika ushawishi wenu.”3

”Tunataka nyumba zetu zibarikiwe na akina dada wasomi wa maandiko—hata kama ujaolewa au umeolewa, kijana ua mzee, mjane au unaishi katika familia. Mmwe wasomi wa maandiko—sio kuwaweka wengine chini, lakini kuwainua juu!”4

Rais Spencer W. Kimball (1895–1985).

Muhtasari

  1. Julie B. Beck, “My Soul Delighteth in the Scriptures,” Liahona May 2004, 107–9.

  2. Thomas S. Monson, “Three Goals to Guide You,” Liahona, Nov. 2007, 118.

  3. Spencer W. Kimball, “Privileges and Responsibilities of Sisters,” Ensign, Nov. 1978, 102.

  4. Spencer W. Kimball, “The Role of Righteous Women,” Ensign, Nov. 1979, 102.

Usaidizi kwa Mwalimu Mtembelezi

Wakati wa matembezi, jibu maswali na shirikisha utambuzi ukitumia maandiko. Toa ushuhuda wa jinsi mafundisho ya maandiko yameimarisha imani yako. Muulize dada unayemtembelea kushirikisha jinsi kusoma kwake kwa maandiko kumeimarisha nyumba yake na familia yake.

Matayarisho ya Kibinafsi

Yohana 5:39

2 Timotheo 3:1–17

2 Nefi 9:50–51; 31:20; 32:3–5

M&M 138:1–11