2010
Jukumu letu ni Kutunza Kizazi Kinachochipuka
Septemba 2010


Ujumbe wa Mwalimu Mtembelezi, Septemba 2010

Jukumu letu ni Kutunza Kizazi Kinachochipuka

Soma kifaa hiki, na kama inavyostahili kizungumzie pamoja na kina dada unaowatembelea. Tumia maswali ili kukusaidia kuwaimarisha dada zako na kuufanya Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama kuwa sehemu hai ya maisha yako mwenyewe.

Relief Society seal

Imani • Familia • Usaidizi

Kutoka kwa maandiko

Methali 22:6; Waefeso 6:4; Enoshi 1:1; Alma 53:20–21; 56:47; 57:27

Pasipokuwa na utunzaji, kizazi chetu kinachochipuka kinaweza kuwa katika hatari ya kuwa kama kilichoelezewa katika Mosia 26. Vijana wengi hawakuamini mila za babu zao na wakawa watu tofauti katika imani yao, wakibakia hivyo maisha. Kizazi chetu kinachochipuka kinaweza vivyo hivyo kupotoshwa kama hawafahamu sehemu yao katika mpango wa Baba wa Mbinguni

Kwa hivyo ni nini ambacho kitakacho kiweka kizazi kinachochipuka salama? Katika Kanisa, tunafunza kanuni za kuokoa, na hizo kanuni ni kanuni za familia, kanuni ambazo zitasaidia kizazi kinachochipuka kuanza familia, kufunza familia, na kutayarisha familia kwa ibada na maagano—na kisha kizazi kifuatacho kitafunza kinachofuata na vivyo hivyo.

Kama wazazi, viongozi, na washiriki wa Kanisa, tunatayarisha kizazi hiki kwa beaka za Ibrahimu, kwa hekalu. Tuna jukumu la kuwa wazi kabisa juu mambo muhimu ya mafundisho yanayopatikana kwenye tamko kwa familia. Umama na ubaba ni nafasi na majukumu ya milele. Kila mmoja wetu anabeba jukumu la kiume au kike la nusu ya mpango huu.

Tunaweza kufunza fundisho hili katika hali yoyote. Lazima tuongee kwa heshima juu ya ndoa na familia. Na kutoka kwa mfano wetu, kizazi kinachochipuka kinaweza kupata matumaini makuu na kufahamu—sio tu kutoka kwa maneno tunayoyasema bali kutokana na njia tunavyohisi na roho ya familia inavyoonekana.

Julie B. Beck, Rais wa Urais mkuu wa Muungano wa Usaidizi wa akina Mama

Kutoka kwa Historia Yetu

Akihutubia kina dada katika mkutano mkuu wa Muungano wa Usaidizi wa akina Mama wa Septemba 23, 1995, Rais Gordon B. Hinckley alisema: “Ulimwengu tulioomo ni ulimwengu wa mashaka, thamani zinazobadilika. Sauti kubwa zinaitana kwenye kitu kimoja au kingine katika kusaliti viwango vya tabia ambavyo vimejaribiwa kwa miaka mingi”.1 Rais Hinckley kisha akaendelea mbele na kuzindua kwa kina dada, Kanisa, na hatimaye watu kila mahali “Familia: Tamko kwa Ulimwengu”

Katika miaka iliyofuata hii taarifa ya kinabii imetafsiriwa katika lugha nyingi na kusambazwa kwa viongozi wa ulimwenngu. Inawauliza wanainchi na viongozi wa serikali “kuendeleza mikakati iliotengenwzwa ili kudumisha na kuimarisha familia kama sehemu ya msingi ya jamii”2

Tamko limekuwa msingi wa imani kwa watakatifu wa siku za mwisho kuhusu familia, matamshi ambayo tunaweza kushikilia kwa nguvu na kujua kwamba kwa kuishi mafunzo yake, tunaimarisha familia na nyumba zetu.

Muhtasari

  1. Gordon B. Hinckley, “Stand Strong Against the Wiles of the World,” Ensign, Nov. 1995, 99.

  2. Ona “Familia: Tamko kwa Ulimwengu,” Liahona, Oct. 2004, 49.

Ninaweza Kufanya Nini?

  1. Ninawezaje kuwasaidia dada zangu kutumia “Familia: Tamko kwa Ulimwengu” kutunza kizazi kinachochipuka? Unaweza kufikiria kushikirisha nakala ya tamko hili na kuwasaidia dada zako kutambua na kuweka alama kwenye vifungu ambavyo vitaweza kufunza vyema mafundisho muhimu.

  2. Ninaweza vipi kutunza kizazi kinachochipuka? Unaweza kufikiria kuwafikia washiriki wa kata na tawi lako, familia, au jamii ambayo inaweza kunufaihika kutokana na uangalifu na upendo wako.