Vijana
Tazama Wakati Ujao
Wavulana wengi hujitayarisha kifedha ili kuhudumu misheni Katika Afrika sehemu ya matayarisho hayo ni kupata fedha za kutosha kulipia pasi Sedrick Tshiambile alijipatia kile alichohitaji kwa njia ya ubunifu: kwa kuuza ndizi kwa baisikeli.
Sedrick anaishi Luputa, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Ni mmojawapo wa wavulana 45 katika wilaya ya Luputa ambao wanafanya kazi kuweka akiba ya kulipia pasi ili kuenda misheni. Katika DR Congo pasi inagharimu $250, ambayo ni karibu theluthi mbili za gharama ya kujenga nyumba.
Lakini Sedrick hakukata tamaa Alipata fedha zake za misheni kwa kuendesha baisikeli kilometa 15–30 (maili 9–19) kutoka Luputa hadi vijiji vidogo, ambapo alinunua ndizi, kisha kuendesha besikeli tena kupiatia kwenye sehemu joto ya Afrika ya nyasini, besikeli yake ikiwa imebeba sana matunda ya kuuza jijini. Kila juma usafiri karibu kilometa 180 (maili 112) kwenye barabara ya mchanga changarawe, na ni wakati mmoja tu ameangusha mzigo wake.
Kwa juhudi zake Sedrick aliweza kupata karibu $1.25 kwa juma au $65.00 kwa mwaka. Ilimchukua miaka minne kuweka akiba ya kutosha kulipia pasi yake, lakini sasa anajua maisha yake yatajumuisha misheni kwa sababu yeye yu tayari kifedha tayari kujibu wito wa kuhudumu.