2011
Historia na Urithi wa Muungano wa Usaidizi wa kina Mama
Januari 2011


Ujumbe wa Mwalimu Mtembelezi, Januari 2011

Historia na Urithi wa Muungano wa Usaidizi wa kina Mama

Soma kifaa hiki, na kama ifaavyo, ukijadili pamoja na kina dada unaowatembelea. Tumia maswali ili kukusaidia kuwaimarisha dada zako na kuufanya Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama kuwa sehemu hai ya maisha yako mwenyewe.

Relief Society seal

Imani • Familia • Usaidizi

Eliza R. Snow alikumbuka jinsi Nabii Joseph Smith alivyofundisha kwamba “ ingawaje jina [Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama] linaweza kuwa la kisasa, shirika hilo ni la asili ya kale.”1

Baba wa Mbinguni na Mwanawe, Yesu Kristo, walimtembelea Joseph Smith na, kupitia kwake, walirejesha ujalivu wa injili duniani. Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama ulikuwa sehemu ya urejesho huo. Mpangilio wa Kanisa haukuwa kamili hadi wakati kina dada walipopangiliwa.2

Katika miezi ijayo, kila Ujumbe wa Mwalimu Mtembelezi utatupatia fursa ya kujifunza mengi kuhusu historia ya Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama na sehemu yake katika injili rejesho. Kwa sababu nyingi, kuelewa historia yetu si muhimu tu bali ni lazima.

Kwanza, kuelewa historia yetu inatupatia motisha kuwa wanawake wa Mungu tunaohitajika kuwa. Kwa kufuata mifano miema ya wanawake wadilifu wa Watakatifu wa Siku za Mwisho, tunaweza kujifunza kutoka kwa historia jinsi ya kukumbana na maisha ya baadaye.3

Pili, historia yetu inafundisha kwamba kanuni zilezile zilizokuwemo katika Kanisa la Zamani ndizo kanuni zetu za msingi leo. Elimu hii na dhamira yetu—ya kuongeza imani na utakatifu wa kibinafsi, inaimarisha familia na nyumba, na kusaidia wale wenye mahitaji—kutengeneza uhusiano kati ya maisha yetu ya zamani na sasa.

Tatu, tunavyothamini historia yetu, tunaweza kushiriki vyema urithi wetu wa kiroho. Rais Henry B. Eyring, Mshauri wa Kwanza katika Urais wa Kwanza, alisema: “Unapasha urithi siku zote unapowasaidia wengine kupokea karama ya wema. … Historia ya Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama imeandikwa kwa maneno na nambari, lakini urithi unapashwa moyo hata moyo.”4

Hatimaye, kuelewa historia yetu inasaidia kutufanya sehemu hai ya maisha yajayo ya Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama. Rais Spencer W. Kimball (1895–1985) alielezea, “Tunajua kwamba wanawake wenye shukrani sana kwa maisha yaliyopita watajishughulisha na utengenezaji wa maisha matakatifu.”5

Julie B. Beck, Rais mkuu wa Muungano wa Usaidizi wa akina Mama.

Kutoka kwa Maandiko

Esta 9:28–29; Warumi16:1–2; Alma 37:8; Moroni 7:45–47

Kutoka kwa Historia Yetu

“Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama ni shirika la Bwana kwa wanawake.”6 Katika wadhifa wake kama nabii, Joseph Smith alitengeneza Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama mnamo Machi 17, 1842. Kundi ndogo, tofauti katika mkutano huo wa kwanza walikuwa wanawake waliojitolea kwa dhati, linalofanana na kina dada wa Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama leo. “Wadogo zaidi walikuwa ni vijana watatu, na mkongwe zaidi, alikuwa ni mwanamke katika umri wake wa hamsini. Kumi na moja ya wanawake waliolewa, wawili walikuwa wajane, sita wao hawakuwa wameoleka, na hali ya ndoa ya mmoja wao haijulikani. Elimu yao na maisha yao yalikuwa tofauti sana, kama vile hali zao za kiuchumi. Uanuwai wao ilizidi kupanuka mara nyingi jinsi uanachama wa shirika ulivyoendelea kukua, lakini walikuwa na wangeendelea kuwa kitu moja.”7

Muhtasari

  1. Eliza R. Snow, “Female Relief Society,” Deseret News, Apr. 22, 1868, 81.

  2. Ona Teachings of Presidents of the Church: Joseph Smith (2007), 451.

  3. Ona L. Tom Perry, “The Past Way of Facing the Future,” Liahona, Nov. 2009, 73–76.

  4. Henry B. Eyring, “The Enduring Legacy of Relief Society,” Liahona, Nov. 2009, 124–25.

  5. Spencer W. Kimball, “Privileges and Responsibilities of Sisters,” Ensign, Nov. 1978, 104.

  6. Spencer W. Kimball, “Relief Society—Its Promise and Potential,” Ensign, Mar. 1976, 4.

  7. Jill Mulvay Derr, Janath Russell Cannon, na Maureen Ursenbach Beecher, Women of Covenant (1992), 28.