Ujumbe wa Urais wa Kwanza, Januari 2011
Bwana Anahitaji Wamisionari
Oktoba iliyopita katika mkutano mkuu niliagiza wamisionari zaidi. Kila mvulana mwenye kustahiki, mwenye afya njema anafaa kujitayarisha kuhudumu katika misheni. Huduma kama hiyo ni jukumu la ukuhani— sharti ambalo Bwana anatarajia kutoka kwetu sisi ambao tumepewa mengi sana. Vijana, nawasihi mjitayarishe kwa huduma kama wamisionari. Jiwekeni wasafi na halisi na wenye kustahiki kumwakilisha Bwana. Dumisha afya na nguvu zako Jifunze maandiko Pale ambapo inapatikana, shiriki katika seminari na chuo. Jifahamishe kijitabu cha maelekezo cha mmisionari Preach My Gospel.
Kina dada, ingawaje hamna majukumu sawa sawa na ya ukuhani kama vile wavulana ya kuhudumu kama wamisionari, nyinyi pia mnaweza kufanya mchango wa dhamani kama wamisionari, na tunakaribisha huduma yenu.
Kwa kina kaka na dada waliokomaa katika kanisa, nawakumbusha kwamba Bwana anahitaji wengi, wengi zaidi wenu kuhudumu kama wamisionari. Kama hamjafikia wakati wenu katika maisha wa kuhudumu kama wamisionari, nawasihi mjitayarishe sasa kwa ile siku, kama hali itawawezesha, wewe na mwenzi wako mnaweza kufanya hivyo. Kuna nyakati chache katika maisha yako ambapo utaweza kufurahia roho mwema na kuridhika ambako kunatokana na kutoa huduma ya pamoja katika kazi ya Bwana.
Sasa, kati yenu mnaweza kuwa wenye haya kwa asili au mnajifikiria kuwa hamwezi kutenda kikamilifu katika wito wa kuhudumu. Kumbuka kwamba hii ni kazi ya Bwana, na wakati tunapokuwa katika kazi ya Bwana, tuna haki ya usaidizi wa Bwana. Bwana atawezesha mgongo kubeba mzigo uliowekwa juu yake.
Wengine, ingawaje mu wastahiki kuhudumu, mnaweza kuhisi kuwa na kipa umbele muhimu sana Kweli nakumbuka ahadi ya Bwana: “Kwa maana wao wanaoniheshimu nitawaheshimu” (1 Samweli 2:30). Hakuna kati yetu watakaomheshimu Baba yetu wa Mbinguni na Mwokozi wetu zaidi ya kuliko kuhudumu kama wamisionari kujitolea na wenye fadhili.
Kama mfano wa huduma kama hiyo ilikuwa ni uzoefu wa Juliusz na Dorothy Fussek, ambao waliitwa katika misheni huko Poland. Ndugu Fussek alizaliwa huko Poland Aliongea lugha ya huko. Aliwapenda watu wa huko. Dada Fussek alizaliwa Uingereza na alijua machache kuhusu Poland na watu wake. Wakimtumainia Bwana, walianza kazi yao kazi ilikuwa na upweke, jukumu lao lilikuwa kuu. Misheni ilikuwa wakati huo haijaandaliwa katika Poland kazi waliopatiwa Fussek ilikuwa ya kutayarisha njia ili misheni iweze kuaandaliwa.
Je! Mzee na Dada Fussek walivunjika moyo kwa sababu ya uzito wa kazi yao? Hata kwa dakika moja kamwe. Walijua wito wao ulikuwa kutoka kwa Mungu Waliomba kwa usaidizi mtakatifu wake, na walijitolea wenyewe kwa moyo wao wote katika kazi yao.
Wakati ukafika ambapo Mzee Russell M. Nelson wa Jamii ya Mitume Kumi Wawili; Mzee Hans B. Ringger, wakati huo alikuwa wa Wale Sabini; wakiandamana na Mzee Fussek, walikutana na waziri wa mambo ya dini, Adam Wopatka, katika Serikali ya Poland Tulimsikia akisema, “Kanisa lenu limekaribishwa hapa. Mnaweza kujenga majengo yenu; mnaweza kuwaleta wamisionari wenu. Mtu huyu,” akimuonyesha kwa kidole Juliusz Fussek, “amehudumia kanisa lenu vyema. Tunashukuru kwa mfano wake na kazi yake.”
Kama Fussek, acheni tufanye kile tunachofaa kufanya katika kazi ya Bwana. Basi tunaweza, pamoja na Juliusz na Dorothy, wakirudia Zaburi:
“Msaada wangu u katika Bwana, aliyezifanya mbingu na nchi.
“… asisinzie akulindaye.
“Naam, hatasinzia wala hatalala usingizi, Yeye aliye mlinzi wa Israeli” (Zaburi 121:2–4).
© 2011 na Intellectual Reserve, Inc. Haki zote zimehifadhiwa Imechapishwa USA Kiingereza kiliidhinishwa: 6/10. Tafsiri iliidhinishwa: 6/10. Tafsiri ya First Presidency Message, January 2011. Swahili. 09761 743