2013
Kazi ya Umisionari
Januari 2013


Ujumbe wa Mwalimu Mtembelezi, Januari 2013

Kazi ya Umisionari

Soma kifaa hiki kwa maombi na kama ifaavyo, ukijadili pamoja na kina dada unaowatembelea. Tumia maswali ili kukusaidia kuwaimarisha dada zako na kuufanya Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama kuwa sehemu hai ya maisha yako mwenyewe. Kwa taarifa zaidi, nenda kwenyewww.reliefsociety.lds.org.

Picha
Alama ya Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama

Imani, Familia, Usaidizi

Watakatifu wa Siku za Mwisho wanatumwa “kufanya kazi katika shamba lake la mzabibu kwa ajili ya wokovu wa roho za wanadamu” (M&M 138:56), ambayo inajumuisha kazi ya umisionari. Hatuitajiki kuwa katika misheni rasmi ili kushiriki injili. Wengine ambao maisha yao yamebarikiwa na injili wako karibu nasi, na tunapojitayarisha, Bwana atatumia sisi. Waalimu watembelezi wanaweza kuchukua majukumu yao ya kiroho na kusaidia “kuleta kutokufa na uzima wa milele wa mwanadamu” (Musa 1:39).

Wakati Nabii Joseph Smith aliasisi Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama mnamo 1842, alisema kwamba wanawake hawapaswi tu kuwatunza masikini bali pia kuokoa nafsi.1 Hili bado ndilo dhumuni letu.

“Bwana … hukabidhi ushuhuda wa kweli kwa wale ambo wataushiriki na wengine” alisema Rais Dieter F. Uchtdorf, Mshauri wa Pili katika Urais wa Kwanza. “Hata zaidi, Bwana hutarajia washiriki wa Kanisa Lake ‘kufungua [vinywa vyao] nyakati zote, wakitangaza injili [Yake] kwa sauti ya kufurahi’ (M&M 28:16). … Wakati mwengine kishazi kimoja cha ushuhuda kinaweza kuanzisha matukio ambayo yataathiri maisha ya mtu kwa umilele.”2

Kutoka kwa Maandiko

Mafundisho na Maagano 1:20–23; 18:15; 123:12

Kutoka kwa Historia Yetu

Hadithi ya Olga Kovářová wa kutoka iliyokuwa Chekosolvakia ni mafano wa kazi ya mmisionari mshiriki kutoka kwa historia ya Muungano wa Usiadizi wa Kina Mama wetu. Katika miaka ya 1970, Olga alikuwa wanafunzi wa udaktari wa falsafa na mwenye njaa ya maisha ya kiroho cha kina. Alimwona Otakar Vojkůvka wa miaka 75, Mtakatifu wa Siku za Mwisho. “Yeye alionekana kwangu kuwa wa umri wa miaka 75 lakini katika moyo wake kuwa miaka 18 na mwenye ujalivu wa shangwe,” alisema.“Hii haikuwa kawaida katika Chekosolvakia katika wakati huu wa ubeuzi.”

Olga alimuuliza Otakar na familia yake jinsi walipata shangwe. Wao walimjulisha yeye na washiriki wengine wa Kanisa na kumpatia Kitabu cha Mormoni. Akakisoma kwa hima na punde akabatizwa na kutibitishwa. Kutoka wakati huo Olga amekuwa na ushawishi kwa wema katika ulimwengu wa ugandamizi wa kisiasa na mateso ya kidini. Alihudumu kama Rais wa Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama katika tawi lake dogo na kusaidia nafsi za wengine kwa kuwaleta kwa Kristo.3

Muhtasari

  1. Ona Teachings of Presidents of the Church: Joseph Smith (2007), 453.

  2. Dieter F. Uchtdorf, “Waiting on the Road to Damascus,” Liahona, May 2011, 76–77.

  3. Ona Daughters in My Kingdom: The History and Work of Relief Society (2011), 92–95.

Chapisha