2013
Sauti ya Bwana
Januari 2013


Ujumbe wa Urais wa Kwanza, Januari 2013

Sauti ya Bwana

Picha
Na Rais Henry B. Eyring

Mafundisho na Maagano hualika watu wote kila mahali kusikia sauti ya Bwana Yesu Kristo (ona M&M 1:2, 4, 11, 34; 25:16). Kimejaa na ujumbe Wake, maonyo, na ushawishi wa kutia moyo uliotolewa kwa ufunuo kwa manabii wateule. Katika hizi funuo tunaweza kuona jinsi Mungu anaweza kujibu maombi yetu ya imani kwa jumbe za maelekezo, amani, na maonyo.

Katika maombi yetu tunatafuta kujua kile Mungu anataka sisi tufanye, kile tunapaswa kufanya ili tupate amani na furaha katika maisha haya na yajayo, na kile kilicho mbele yetu. Mafundisho na Maagano yamejaa majibu ya maswali kama hayo yanayoulizwa na watu wa kawaida na manabii katika maombi ya unyenyekevu. Kinaweza kuwa mwongozo wa thamani wa kutufunza jinsi ya kupokea majibu ya maswali kuhusu hali njema ya muda na wokovu wa milele.

Unyenyekevu na imani katika Bwana Yesu Kristo ni muhimu. Oliver Cowedry alipokea jibu kutoka kwa Bwana kuhusu hamu yake ya kutaka kusaidia katika tafsiri ya Kitabu cha Mormoni: “Kumbuka kwamba pasipo imani huwezi kufanya lolote; hivyo basi omba kwa imani. Usicheze na mambo haya; usiombe kitu kile usichopaswa kukiomba” (M&M 8:10).

Tena na tena katika Mafundisho na Maagano, Bwana huhitaji imani na unyenyekevu kabla Yeye kutoa usaidizi Wake. Sababu moja ya haya ni kwamba majibu Yake yanaweza yasije katika njia tunayotarajia. Wala kila mara hayatakuwa rahisi kukubalika.

Historia ya Kanisa na uzoefu wa wahenga wetu inaonyesha uhalisi huu. Babu yangu mkuu Henry Eyring aliomba kwa dhati ili kujua kile anachopaswa kufanya wakati aliposikia injili ya urejesho iliyofunzwa mnamo 1855. Jibu likaja katika ndoto.

Aliota kwamba alikuwa amekaa mezani pamoja na Mzee Erasrus Snow wa Jamii ya wale Mitume Kumi na Wawili na pamoja na mzee aliyejulikana kama William Brown. Mzee Snow alifunza kanuni za injili kwa kile kilichoonekana kama muda wa saa moja. Kisha Mzee Snow aksema, “Katika jina la Yesu Kristo nakuamuru wewe ubatizwe na huu mtu [Mzee Brown] atakubatiza wewe.”1 Familia yangu inashukrani kwamba Henry Eyring alikuwa na imani na unyenyekevu wa kubatizwa saa 1:30 asubuhi katika kidibwi cha maji ya mvua katika St. Louis, Missouri, USA, na Mzee Brown.

Jibu la maombi yake halikuja kwa sauti ya kusikika kutoka kwa Bwana. Lilikuja katika ono na ndoto usiku, kama ilivyokuwa kwa Lehi (ona 1 Nefi 8:2).

Bwana ametufunza sisi kwamba majibu yanaweza kuja pia kama hisia. Katika Mafundisho na Maagano, Yeye alimfunza Oliver Cowdery, “Tazama, nitakujulisha wewe akilini mwako na katika moyo wako, kwa njia ya Roho Mtakatifu, ambaye atakujia na ambaye atakaa moyoni mwako” (M&M 8:2).

Na Yeye alimtia moyo Oliver kwa njia hii: “Sikusema amani akilini mwako kuhusiana na jambo hili? Ni ushahidi gani mkubwa zaidi unaoweza kupata kuliko kutoka kwa Mungu?” (M&M 6:23).

Mafundisho na Maagano, Historia ya Kanisa, na historia ilyowekwa na Henry Eyring katika misheni yake punde baada ya ubatizo wake imenifunza kwamba majibu yanaweza kuhisika kama maonyo pia kama amani.

Mnamo Aprili 1857, Mzee Parley P. Pratt wa Jamii ya wale Mitume Kumi na Wawili alihudhuria mkutano mkuu katika pale ambapo sasa ni Oklahoma, USA. Henry Eyring aliandika kwamba akilini mwa Mzee Pratt “zilijawa na ubashiri wa hofu … , asiweze kutambua siku za usoni wala njia ya kutorokea.”2 Henry aliandika habari za huzuni mara moja muda kidogo baada ya kifo cha kishahidi cha Mtume. Mzee Pratt alikuwa amesonga mbele katika safari yake licha ya hisia za hatari, kama vile Nabii Joseph alivyokuwa amefanya alipoenda kule Carthage.

Ni ushuhuda wangu kwamba Bwana daima hujibu maombi ya imani ya unyenyekevu. Mafundisho na Maagano na uozefu wetu wa kibinafsi hutufunza jinsi ya kutambua majibu hayo na kuyakubali kwa imani, iwe ni maelekezo, uthibitisho wa kweli, au maonyo. Naomba kwamba daima tusikilize na kutambua sauti ya upendo ya Bwana.

Muhtasari

  1. “The Journal of Henry Eyring: 1835–1902” (mswaada ambao haujachapishwa unaomikiwa na mwandishi).

  2. “The Journal of Henry Eyring: 1835–1902.”

Kufundisha kutoka kwa Ujumbe huu

1. Fikiria kusoma kwa pamoja aya zinazohusu maombi katika ujumbe huu. Mnaposoma, waulize wanafamilia kusikiliza kwa makini jinsi Mungu hujibu maombi. Fikiria kushuhudia umuhimu wa maombi.

2. Mafundisho na Maagano yamejaa majibu ya maswali yanayoulizwa na watu katika maombi. Ingekuwaje kama majibu ya maswali yao (funuo) hayangeandikwa kamwe? Ihimize familia kujifunza kutambua na kufuata msukumo wa Roho. Wanaweza kuandika mawazo yao kuhusu maombi katika shajara zao.

Chapisha