2013
Niliweza Kuachilia huzuni wangu
Septemba 2013


Vijana

Niliweza Kuachilia huzuni wangu

Mtunzi anatoka Taiwani.

Wakati rafiki yangu Ndugu Chen na mke wake walibatizwa katika kata yetu, nilijawa na furaha sana. Mwaka baada ya ubatizo wao, walifunganishwa hekaluni, na mtoto wao aliyekuwa amefariki kabla ya kujiunga na Kanisa aliunganishwa nao. Ilikuwa inastaajabisha kuona familia ya Chen ikikua katika injili.

Kisha Ndugu Chen aliuawa katika ajali ya gari mwaka uliofuata. Baada ya ajali, kifo chake kilionekana kuwa katika akili yangu na mara nyingi nilitishwa na ndoto zangu. Niliamka nikiwa na machozi na kuuliza tena na tena, “Kwa nini? Kwa nini Bwana huruhusu aina hii ya mateso kutokea? Kwa nini vitu kama hivi vitokee kwa familia hii nzuri? Siku moja, nilipokuwa nahangaika na maswali haya, Nilichukua kitabu cha kiada cha somo na kusoma maneno haya kutoka kwa Rais Spencer W. Kimball (1895–1985):

“Kama tungeangalia maisha ya muda kama kuishi kote, basi maumivu, huzuni, kushindwa, na maisha mafupi yangekuwa shida kubwa. Lakini kama tutayaangalia maisha kama kitu cha milele kilichotanuka mbali katika maisha kabla ya maisha haya na katika hali ya milele ya kifo inayokuja, hivyo yale yote yanayotokea yanaweza kuwekwa katika mtazamo sahihi. …

“Je! Hatujawekwa wazi katika majaribu ili kujaribu uwezo wetu, magonjwa ili tujifunze uvumilivu, kifo ili tuweze kupata maisha ya milele na kuinuliwa?”1

Kwa wakati huo, niliamua kuachana na huzuni wangu na kutazama katika hali ijayo iliyoahidiwa na inayowezekana. Niliona katika macho yangu ya akili Ndugu Chen akiungana kwa furaha na familia yake. Upeo huo uliniletea amani. Ninajua kuwa Baba wa Mbinguni atatupatia hekima na ujasiri ya kuzikabili dhiki.

Muhtasari

  1. Teachings of Presidents of the Church: Spencer W. Kimball (2006), 15.

Chapisha