2013
Watakatifu kwa Misimu Yote
Septemba 2013


Ujumbe wa Urais wa Kwanza, Septemba 2013

Watakatifu kwa Majira Yote

Picha
Rais Dieter F. Uchtdorf

Nina kumbukumbu ya utotoni ya sehemu ya dunia ambayo inaweza kutumika kama picha ya postikadi kwa ajili ya majira yanayobadilika ya mwaka. Kila mwezi unaopita ulikuwa mtukufu na wa kushangaza. Wakati wa siku kamilifu ya majira ya baridi, theluji kamili ilifunika milima na mitaa ya mji. Majira ya kuchipua yalileta mvua za kusafisha na mlipuko wa maisha yaliyovishwa kijani. Anga zembe ya majira ya joto ilitumika kama turubai la samawati zuri kwa ajili ya mwangaza wa jua angavu. Na majira ya kustaajabisha ya kupukutika majani yalibadilisha asili katika rangi angavu za chungwa, njano, na nyekundu. Kama mtoto, nilipenda kila majira, na mpaka leo, ninapenda hali na upekee wa kila moja yake.

Vile vile tuna majira katika maisha yetu. Mengine ni ya vuguvugu na yanapendeza. Mengine hayako hivyo. Siku nyingine maisha yetu ni mazuri kama picha katika kalenda. Na bado kuna siku na hali ambazo husababisha moyo kuuma na inaweza kuleta hisia za kukatisha tamaa katika maisha yetu, ubishi, na uchungu.

Nina uhakika wakati mmoja au mwingine tumefikiria kwamba ingekuwa vizuri kuwa na makazi katika ardhi iliyojawa tu na picha majira ya picha kamilifu na kuepuka nyakati mbaya katikati yake.

Lakini hii haiwezekani. Wala haipendelewi.

Ninavyoangalia kwenye maisha yangu, ni dhahiri kwamba nyakati nyingi za ukuaji mkubwa umenijia wakati nilipokuwa nikipitia kwenye majira ya dhoruba.

Baba yetu wa Mbinguni mwenye hekima zote alijua kwamba ili watoto Wake waweze kukua hata kuwa viumbe walivyosanifiwa kuwa, wangehitaji kupata uzoefu wa shida wakati wa safari katika maisha ya muda. Lehi, nabii wa Kitabu cha Mormoni alisema bila kupingwa, “haki isingekuja” (2 Nefi 2:11). Hakika, ni machungu ya maisha ambayo hutusaidia kutambua, kulinganisha, na kufurahia utamu wake (ona M&M 29:39; Musa 6:55).

Rais Brigham Young alisema hivi: “Kila kiumbe chenye akili kilichovishwa na mataji ya utukufu, kutokufa, na maisha ya milele lazima wapitie kwenye jaribio lilichaguliwa kwa ajili ya viumbe wenye akili kupitia, ili kupata utukufu na kuinuliwa. Kila janga ambalo huja katika viumbe wa kuharibika litapitiwa ili kuwaandaa kufurahia uwepo wa Bwana. Kila jaribio na uzoefu ulioupitia ni muhimu katika wokovu wako.”1

Swala siyo kama tutapata uzoefu wa majira ya dhiki lakini ni jinsi tutakavyoshinda dhoruba. Nafasi yetu kubwa wakati wa mabadiliko ya kila mara ya majira ya maisha ni kulishikilia kwa umakini neno aminifu la Mungu, kwani ushauri wake umesanifiwa siyo tu kutusaidia kushinda dhoruba za maisha lakini pia kutuongoza kuzipita dhoruba. Baba yetu wa Mbinguni ametupatia neno lake kupitia manabii Wake—ufahamu wa thamani ulisanifiwa kutuongoza kutoka katika changamoto za majira magumu kuelekea kwenye furaha isiyoelezeka na mwanga mzuri wa maisha ya milele. Ni sehemu muhimu ya uzoefu wa maisha, kujenga nguvu, ujasiri, na uadilifu kuushikilia ukweli na haki bila kujali mapigo tunayoweza kuyapata.

Wale walioingia katika maji ya ubatizo na kupokea kipawa cha Roho Mtakatifu wameweka miguu yao katika njia ya ufuasi na wamepewa jukumu la kufuata kwa udhabiti na kwa imani katika njia za Mwokozi wetu.

Mwokozi alifundisha kwamba jua huchomoza “katika mazuri na mabaya, na … na mvua huwanyeshea wenye haki na wasio na haki” (Mathayo 5:45). Wakati mwingine hatuwezi kuelewa kwa nini vitu vigumu, hata visivyo na haki, hutokea katika maisha. Lakini kama wafuasi wa Kristo, tutaamini kwamba kama “tutatafuta kwa bidii, kusali kila mara, na kuamini, … kila kitu kitafanya kazi pamoja kwa ajili ya wema wetu, kama tutatembea wima” (M&M 90:24; mkazo imeongezwa).

Kama washiriki wa Kanisa Lake, kama Watakatifu, tunahudumia kwa furaha na kiutashi katika hali zote na katika majira yote. Na tunavyofanya hivyo, mioyo yetu huwa inajazwa na imani takatifu, tumaini linaloponya, na hisani ya kimbinguni.

Hata hivyo, tunatakiwa kupitia kwenye majira yote—mazuri na yale yenye machungu. Lakini haijalishi majira gani, kama wafuasi wa Yesu Kristo, tutapumzisha tumaini letu Kwake tunapotembea kuelekea kwenye nuru Yake.

Kwa kifupi, sisi ni Watakatifu wa Mungu, tulioazimia kujifunza kutoka Kwake, kumpenda Yeye, na kuwapenda wenzetu. Tuna hija katika barabara iliyobarikiwa ya ufuasi, na tutatembea kwa udhabiti katika malengo yetu ya mbinguni.

Hivyo, na tuwe Watakatifu katika majira ya kuchipua, majira ya joto, majira ya majani kupuputika, na majira na baridi. Na tuwe Watakatifu majira yote.

Muhtasari

  1. Teachings of Presidents of the Church: Brigham Young (1997), 261–62.

Kufundisha kutoka kwa Ujumbe huu

Urais wa Kwanza umefundisha, “Baadhi ya mafundisho makubwa yamefundishwa katika kuimba nyimbo” (Hymns, ix). Unapojadili ujumbe huu, fikiria kuimba na wale unaowafundisha moja ya nyimbo hizi au nyimbo nyingine kuhusu kuvumilia dhiki: “How Firm a Foundtion” (no. 85); “The Lord Is My Shepherd” (no. 108); au “Let Us All Press On” (no. 243). Kama utahisi maongozo, waelezee jinsi majira ya dhoruba katika maisha yako yaligeuka kuwa baraka.

Chapisha