2013
Kujitegemea
Septemba 2013


Ujumbe wa Mwalimu Mtembelezi, Septemba 2013

Kujitegemea

Soma nyenzo hii kwa maombi na kama ifaavyo, ukijadili pamoja na kina dada unaowatembelea. Tumia maswali ili kukusaidia kuwaimarisha dada zako na kuufanya Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama kuwa sehemu hai ya maisha yako mwenyewe. Kwa taarifa zaidi, nenda kwenye reliefsociety.lds.org.

Picha
Nembu ya Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama

Imani, Familia, Usaidizi

Kujitegemea ni uwezo, sharti, na juhudi za kukidhi mahitaji ya kiroho na ya muda wetu wenyewe na kwa familia zetu.1

Tunapojifunza na kuzitumia kanuni za kujitegemea katika nyumba zetu na jamii, tuna nafasi ya kuwasaidia maskini na walio na mahitaji na kuwasaidia wengine wajitegemee ili waweze kuvumila nyakati za dhiki.

Tuna nafasi na wajibu wa kutumia wakala wetu kuweza kujitegemea kiroho na kimwili. Katika kuzungumzia kujitegemea na utegemezi wetu kwa Baba yetu wa Mbinguni, Mzee Robert D. Hales wa Jamii ya Mitume Kumi na Wawili amefundisha: “Tunakuwa tumeongolewa na kuwa wenye kujitegemea kiroho tunapoyaishi maagano yetu—kwa maombi kupitia ustahili wa kupokea Sakramenti, kustahili sifu ya hekalu, na kujitolea kwa ajili ya wengine.”2

Mzee Hales alitushauri tujitegemee kimwili, “inayojumuisha kupata elimu baada ya shule ya upili au mafunzo ya weledi, kujifunza kufanya kazi, na kuishi kadiri ya uwezo wetu. Kwa kuepuka madeni na kuweka akiba hela sasa, tunajiandaa kuhudumia katika Kanisa muda kamili katika miaka ijayo. Kusudi la kujitegemea kimwili na kiroho ni kujiinua katika ardhi ya juu ili tuweze kuwainua na wenzetu walio na mahitaji.”3

Kutoka kwa Maandiko

Mathayo 25:1–13; 1 Timotheo 5:8; Alma 34:27–28; Mafundisho na Maagano 44:6; 58:26–29; 88:118

Kutoka kwa Historia Yetu

Baada ya Watakatifu wa Siku Za Mwisho kukusanyika katika Bonde la Salt Lake, ambalo lilikuwa ni jangwa lililojitenga, Rais Brigham Young aliwataka wao kujistawisha na kuanzisha makao ya kudumu. Hii ilimaanisha Watakatifu walihitaji ujuzi ambao ungeruhusu kujitegemea. Katika juhudi hizi, Rais Young alikuwa na imani kubwa sana katika uwezo wao, talanta, uaminifu, na utashi wa wanawake, na akawapa moyo katika baadhi ya shughuli maalumu za kimwili. Wakati wajibu huu maalumu wa Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama mara nyingi ni tofauti, kanuni zinabaki zile zile:

  1. Jifunze kupenda kazi na kuepuka uzembe.

  2. Jipatie roho ya kujitolea

  3. Kubali jukumu binafsi kwa ajili ya nguvu za kiroho, afya, elimu, ajira, usimamizi wa fedha, chakula, na mahitaji mengine ya kusaidia maisha.

  4. Sali kwa ajili ya imani na ujasiri kukumbana na changamoto.

  5. Wape nguvu wengine wanaohitaji msaada. 4

Muhtasari

  1. Ona Handbook 2: Administering the Church (2010), 6.1.1.

  2. Robert D. Hales, “Coming to Ourselves: The Sacrament, the Temple, and Sacrifice in Service,” Liahona, May 2012, 34.

  3. Robert D. Hales, “Coming to Ourselves,” 36.

  4. Ona Daughters in My Kingdom: The History and Work of Relief Society (2011), 51.

Ninaweza Kufanya Nini?

  1. Je! Ninawasaidiaje akina dada ninaowatunza kutafuta suluhisho la mahitaji yao ya kimwili na ya kiroho?

  2. Je! Ninaongeza kujitegemea kwangu kiroho kupitia kujiandaa kwa ajili ya Sakramenti na kujitolea dhabihu kutumikia?

Chapisha