Mafundisho ya Wakati Wetu
Mafundisho ya Jumapili ya nne kwa Ukuhani wa Melkizedeki na Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama yatatengwa kwa “Mafundisho ya Wakati Wetu” Kila somo linaweza kutayarishwa kutoka kwa hotuba moja au zaidi kutoka kwa mkutano mkuu wa hivi majuzi (ona chati hapa). Marais wa vigingi na wilaya wanaweza kuchagua hotuba zitakazotumiwa, au wanaweza kuwapangia jukumu hili maaskofu na marais wa matawi. Viongozi wanasisitiza umuhimu wa ndugu wa Ukuhani wa Melkizediki na akina dada wa Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama kusoma hotuba hizo hizo katika Jumapili hizo.
Wale wanaohudhuria mafundisho ya Jumapili ya nne wanahimizwa kusoma na kuleta darasani toleo la gazeti la mkutano mkuu la hivi karibuni.
Mapendekezo ya Kutayarisha Somo kutoka kwa Hotuba
Omba kwamba Roho Mtakatifu awe nawe unaposoma na kufundisha hotuba hizi. Unaweza kushawishika kutayarisha masomo kwa kutumia vifaa vingine, lakini hotuba za mkutano mkuu ni mtaala ulioidhinishwa. Jukumu lako ni kuwasaidia wengine kujifunza na kuishi kulingana na injili kama ilivyofundishwa katika mkutano mkuu wa Kanisa wa hivi majuzi.
Rejelea upya hotuba hizi, ukitafuta kanuni na mafundisho yanayolingana na mahitaji ya washiriki wa darasa. Pia, tafuta hadithi, marejeleo ya maandiko, na matamko kutoka kwa hotuba ambazo zitakazokusaidia kufundisha kweli hizi.
Tayarisha muhtasari wa jinsi ya kufundisha kanuni na mafundisho. Fikiria kujumuisha maswali ambayo yatawasaidia washiriki wa darasa:
-
Angalia kanuni na mafundisho katika hotuba.
-
Tafakari juu ya maana yake.
-
Shiriki uelewa, tajiriba, uzoefu na shuhuda.
-
Tumia kanuni na mafundisho haya katika maisha yao.
Miezi Masomo Yatakapofunzwa |
Vifaa vya Mafundisho ya Jumapili ya Nne |
---|---|
Oktoba 2013–Aprili 2014 |
Hotuba zilizotolewa katika mkutano mkuu wa Oktoba 2013* |
Aprili 2014–Oktoba 2014 |
Hotuba zilizotolewa katika mkutano mkuu wa Aprili 2014* |