2013
Naweza kushiriki Kitabu cha Mormoni?
Desemba 2013


Vijana

Naweza Kushiriki Kitabu cha Mormoni?

Mwandishi anaishi katika Washington ,USA.

Wakati wa mwaka wangu wa kwanza katika shule ya upili, mwalimu wangu wa seminari aliwaalika wanafunzi wa darasa langu wawapaite marafiki zao ambao sio washiriki wa kanisa nakala za Kitabu cha Mormoni. Ingawa nilikuwa mwoga sana, nilikubali mwaliko.

Ilinichukua siku kadha kupata ujasiri, lakini hatimaye nilimpa rafiki yangu Britny kitabu wakati wa chakula cha mchana na nikatoa kwa kifupi ushuhuda wangu. Britny alinishukuru kwa kitabu hicho.

Mwishoni mwa mwaka ule wa shule, Britny aliondoka, lakini tuliendelea kuwasiliana. Alinielezea kuhusu shule yake mpya na jinsi karibu marafiki wake wote walikuwa washiriki wa Kanisa, lakini hakuzungumza kabisa chochote cha kiroho nami.

Yale yalibadilika kabla sijaondoka kwenda kwenye misheni yangu. Nilipata ujumbe kutoka kwa Britny ukisema alikuwa na habari kubwa yangu: atakuwa anabatizwa na alitaka kunishukuru kwa kuwa rafiki yake na kuonyesha mfano mzuri.

Mungu alimchukua mvulana mwenye haya wa umri wa miaka 15 asiyekuwa na ujuzi wowote wa umisionari na akamwelekeza ashiriki injili na mtu fulani aliyejua angeikubali. Ninajua kwamba kwa kumsikiliza Roho, tunaweza kuwapata watu waliotuzunguka wanaongojea kujifunza kuhusu injili ya urejesho. Ninajua kwamba kama tunasaidia kuleta hata mtu mmoja kwa Bwana, ”furaha yetu itakuwa kubwa kiasi gani na yeye katika ufalme wa Baba [yetu]!” (M&M 18:15).

Chapisha