2013
Familia na Marafiki Milele
Desemba 2013


Ujumbe wa Urais wa Kwanza, Disemba 2013

Familia na Marafiki Milele

Picha
Rais Henry B. Eyring

Kokote unakoishi, una marafiki wanaotafuta furaha kuu uliyoipata kwa kuishi injili ya urejesho ya Yesu Kristo. Wanaweza kukosa uwezo wa kuelezea furaha hiyo kwa maneno, lakini wanaweza kuitambua wanapoiona ndani ya maisha yako. Watakuwa na hamu ya kutaka kujifunza chanzo cha furaha hio, hasa wanapoona kwamba unakabiliana na majaribu kama wanavyo kabiliana nayo.

Umeshahisi furaha kadri ulivyo tii amri za Mungu. Hili ni tunda lililoahidiwa kwa kuishi injili (ona Mosia 2:41). Hautii amri za Bwana kwa uaminifu ili uonekane na watu wengine, lakini wale ambao wanachunguza furaha yako wanatayarishwa na Bwana kusikia habari njema ya urejesho wa injili.

Baraka ulizopewa zimeleta majukumu na nafasi za ajabu kwako. Kama mfuasi wa agano la Yesu Kristo, una jukumu la kuwanyooshea wengine nafasi ya kutafuta ongezeko la furaha, hasa kwa marafiki wako na wanafamilia wako.

Bwana aliona nafasi yako na alikuelezea jukumu lako kwa amri hii: “na ni wajibu wa kila mtu ambaye ameonywa amwonye jirani yake” (M&M 88:81).

Bwana anafanya ile amri iwe rahisi zaidi kutii kupitia mabadiliko yanayotokea ndani ya moyo wako unapokubali na kuishi injili ya Yesu Kristo. Na matokeo yake, upendo wako kwa wengine hukua, pia hamu yako ya wao kupata furaha ile ile uliyopata.

Mfano mmoja wa mabadiliko hayo ni jinsi unavyokaribisha nafasi ya kusaidia katika kazi ya Bwana ya umisionari. Wamisionari wa muda punde hujifunza kwamba wanaweza kutarajia jibu la kutia moyo kutoka kwa mwongofu wa kweli kwa ombi la kuelekezwa kwa mwingine. Mwongofu hutamani marafiki na wanafamilia washirikiane nao katika furaha yao.

Wakati kiongozi wa misheni wa kata yako au wamisionari wanapoomba majina ya mtu fulani wa kumfundisha, ni heshima kubwa kwako. Wanajua kwamba marafiki wameona furaha yako na, kwa hivyo marafiki hao wametayarishwa kusikia na kuchagua kuikubali injili. Na wana imani kwamba utakuwa rafiki watakayemhitahi wanapokuja ndani ya ufalme.

Usiwe na hofu kwamba utapoteza marafiki kwa kuwaalika wamisionari kukutana nao. Nina marafiki waliowakataa wamisionari lakini wamenishukuru kwa miaka mingi kwa kuwapatia kitu walijua kilikuwa cha thamani sana kwangu. Unaweza kuwa na marafiki milele kwa kuwapatia injili, ambayo wanaona imekuletea furaha. Usikose nafasi kabisa ya kumwalika rafiki na hasa mwanafamilia kuchagua kufuata mpango wa furaha.

Hakuna nafasi kubwa kwa mwaliko huo kama ndani ya mahekalu ya Kanisa. Hapo Bwana anaweza kutoa ibada za wokovu kwa mababu zetu waliofariki ambao hawakuweza kuzipata walipokuwa hai. Wanakuangalia wewe kwa upendo na mategemeo. Bwana ameahidi kwamba watapata nafasi ya kuja katika ufalme Wake (ona M&M 137:7–8), na amepandikiza upendo kwao ndani ya moyo wako.

Wengi kati yenu mlihisi shangwe mlipofanya ibada za hekaluni kwa ajili ya wengine, sawa na mnavyotoa majina ya watu kwa wamisionari ili wakutane nao. Mmehisi shangwe kubwa kuwafanyia ibada mababu zenu. Ilifunuliwa kwa Nabii Joseph Smith kwamba furaha yetu ya milele inawezekana pale tu tunapotoa njia kwa baraka ile kwa mababu zetu kupitia ibada za hekaluni kwa niaba ya wafu (ona M&M 128:18).

Muda wa Krismasi unageuza mioyo yetu kwa Mwokozi na kwa furaha ambayo injili Yake imetuletea. Tunaonyesha shukrani zetu Kwake vizuri pale tunapotoa furaha ile kwa wengine. Shukrani hugeuzwa kuwa shangwe pale tunapotoa majina kwa wamisionari na tuchukuapo majina ya babu zetu hekaluni. Ule ushahidi wa shukrani zetu unaweza kufanya marafiki na wanafamilia wanaovumilia milele.

Kufundisha kutoka kwa Ujumbe huu

Rais Eyring anaelezea kwamba tunaweza kuonyesha shukrani zetu kwa Mwokozi kwa kushiriki injili na wengine. Unaweza kujadiliana na wale unaowafundisha jinsi zawadi ya injili ilivyobariki maisha yao. Fikiria kuwaalika kwa maombi watambue wale pamoja nao wangependa kushiriki zawadi ya injili na jinsi ambavyo wangefanya hivyo.

Chapisha