2013
Misheni ya Kiungu ya Yesu Kristo: Mwana wa Pekee.
Desemba 2013


Ujumbe wa Mwalimu Mtembelezi, Disemba 2013

Misheni ya Kiungu ya Yesu Kristo: Mwana wa Pekee

Kwa maombi jifunze kifaa hiki na utafute kujua nini cha kushiriki. Kuelewa maisha na ujumbe wa Mwokozi kutaongezaji imani yako Kwake na kubariki wale unaowatunza kupitia ualimu tembelezi? Kwa taarifa zaidi, nenda kwenye reliefsociety.lds.org.

Picha
Nembu ya Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama

Imani, Familia, Usaidizi

Mwokozi wetu, Yesu Kristo, anaitwa Mwana wa Pekee kwa sababu Yeye ni mtu wa kwanza pekee duniani kuzaliwa na mama anayekufa na Baba asiyekufa. Alirithi nguvu za kiungu kutoka kwa Mungu, Baba Yake. Kutoka kwa Mama yake, Mariamu, Alirithi kuweza kufa na aliweza kuwa na njaa, kiu, uchovu, maumivu, na kifo.1

Kwa sababu Yesu Kristo ni Mwana wa pekee wa Baba, Aliweza kuweka chini maisha Yake na kuyachukua tena. Maandiko yanafundisha kwamba “kupitia upatanisho wa Kristo,” sisi “tunapata ufufuo” (Yakobo 4:11). Pia tunajifunza kwamba wote “wanaweza kufufuliwa na kutokufa na kuwa na maisha ya milele” kama “tungeamini” (M&M 29:43).

Tunapokuja kuelewa zaidi inamaanisha nini kwa Yesu kuwa Mwana wa pekee wa Baba, imani yetu katika Kristo itaongezeka. Mzee D, Todd Christofferson wa Jamii ya Mitume Kumi na Wawili alisema, “Imani katika Yesu Kristo ni uthibitisho na uhakika wa (1) Nafasi Yake kama Mwana wa Pekee wa Mungu, (2) Upatanisho Wake usio na mwisho, na (3) Ufufuo Wake wa kweli.”2 Manabii wa sasa wameshuhudia:” [Yesu Kristo] alikuwa Mwana wa Pekee katika mwili wa nyama, Mkombozi wa ulimwengu.”3

Kutoka kwa Maandiko

Yohana 3:16; Mafundisho na Maagano 20:21–24; Musa 5:6–9

Kutoka kwa Historia Yetu

Katika Agano Jipya tunasoma kuhusu wanawake, waliotajwa na wasiotajwa, waliotumia imani katika Yesu Kristo, walijifunza na waliishi kufuatana na mafundisho Yake, na walishuhudia huduma Yake, miujiza Yake, na ukuu Wake. Wanawake hawa wakawa wafuasi wa mfano mwema na mashahidi muhimu katika kazi ya wokovu.

Kwa mfano, Martha alitoa ushuhuda wenye nguvu wa Uungu wa Mwokozi alipomwambia, “Ninaamini kwamba wewe ni Kristo, Mwana wa Mungu, ambaye atakuja Ulimwenguni” (Yohana 11:27).

Baadhi ya mashahidi wa mwanzo wa Uungu wa Mwokozi walikuwa mama Yake, Mariamu, na mpwae Elizabeti. Mara baada ya Mariamu kutembelewa na malaika Gabrieli, alimtebelea Elizabeti. Mara tu Elizabeti aliposikia salamu za Mariamu, “alijazwa na Roho Mtakatifu” (Luka 1:41) na alitoa ushuhuda kwamba Mariamu atakuwa mama kwa Mwana wa Mungu.

Muhtasari

  1. Ona Kanuni za Injili (2009), 52–53.

  2. D. Todd Christofferson, “Building Faith in Christ,” Liahona, Sept. 2012, 13.

  3. “The Living Christ: The Testimony of the Apostles,” Liahona, Apr. 2000, 2–3.

Ninaweza Kufanya Nini?

  1. Kwa nini ni muhimu kwangu mimi kuelewa nafasi za Yesu Kristo?

  2. Imani yetu inaweza kuongezeka vipi tunapoweka maagano yetu?

Chapisha