2014
Wakati Bora wa Kupanda Mti.
Januari 2014


Ujumbe wa Urais wa Kwanza, Januari 2014

Wakati Bora wa Kupanda Mti

Rais Dieter F. Uchtdorf

Katika Roma ya kale, Yanusi alikuwa mungu wa mianzo, mara nyingi alionyeshwa akiwa na nyuso mbili — mmoja ukiangalia nyuma kwa siku zilizopita, mwingine ukiangalia mbele kwa siku za usoni. Lugha zingine hupatia mwezi wa Januari jina lake kwa sababu mwanzoni mwa mwaka ulikuwa ni wakati wa kuwazia na pia wa kupanga.

Maelfu ya miaka baadaye, tamaduni nyingi duniani kote huendeleza tamaduni ya kuweka maazimio kwa ajili ya mwaka mpya. Bila shaka, kuweka maazimio ni rahisi — kuyatimiza ni jambo tofauti kabisa.

Mtu moja aliyekuwa ameweka orodha refu ya maazimio ya Mwaka Mpya alihisi vizuri sana kuhusu maendeleo yake. Aliwaza, “Hadi sasa, nimefuata utaratibu maalum wa lishe, nimetuliza hasira yangu, nimefuata bajeti yangu, na sijalalamika hata mara moja kuhusu umbwa wa jirani yangu. Lakini leo ni Januari 2 na saa ya kengele imelia na ninafaa nitoke kitandani. Itachukua miujiza kuendeleza ufasihi wangu.”

Kuanza Upya

Kuna jambo la kutia tumaini sana kabisa kuhusu mwanzo mpya. Nakisia wakati mmoja au mwingine sote tumetamani kuanza upya na kusahau makosa ya nyuma.

Mimi hupenda kupata kompyuta mpya iliyo na kiendeshi diski kuu kisafi. Kwa muda hufanya kazi vizuri kabisa. Lakini siku na wiki zinavyopita na programu nyingi kuwekwa (baadhi kimaksudi na zingine si kimaksudi vile), hatimaye kompyuta huanza kufanya kazi polepole, na vitu ilivyokuwa ikifanya haraka na kwa ustadi vinaanza kufanywa polepole. Wakati mwingine haifanyi kazi kamwe. Hata kuianzisha inaweza kuwa matanga diski kuu inapojawa na machafuko na mabaki ya taka za kielektroniki. Kuna wakati ambapo suluhisho ya kipekee ni kufomati tena kompyuta na kuanza upya.

Binadamu pia wanaweza kujawa na hofu, wasiwasi, na hatia ya kusumbua. Makosa tuliyofanya (yote kimakusudi na bila kukusudia) yanaweza kutugandamiza hadi ionekane kuwa vigumu kufanya kile tunajua tunapaswa kufanya.

Kwa jambo la dhambi, kuna njia nzuri ya kufomati inayoitwa toba inayoturuhusu kusafisha diski kuu zetu za ndani kutokana na mparaganyo unaogandamiza mioyo yetu. Injili, kupitia Upatanisho wa Yesu Kristo wa kimiujiza na huruma, inatuonyesha njia ya kusafisha nafsi zetu kutokana na mawaa ya dhambi na mara nyingine kuwa mpya, msafi, na asiye na hatia kama mtoto.

Lakini wakati mwingine mambo mengine hutulegeza au kutuzuia, yakileta mawazo na matendo yasiyofaa ambayo hufanya iwe vigumu kwetu kuanza.

Kutoa Ufanisi Wetu

Kuweka malengo ni jambo la busara. Tunajua kwamba Baba yetu wa Mbinguni ana malengo kwa sababu ametuambia kwamba kazi Yake na utukufu ni “kuleta kutokufa na uzima wa milele wa mwanadamu” (Musa 1:39).

Malengo yetu ya kibinafsi yanaweza kutoa ufanisi wetu. Hata hivyo, jambo moja linaloangusha juhudi zetu katika kuweka na kutekeleza maazimio ni kuhairisha. Saa zingine sisi huchelewa kuanza, tukingoja muda bora wa kuanza — siku ya kwanza ya mwaka mpya, mwanzo wa majira ya joto, tutakapoitwa kuwa askofu ama rais wa Muungano wa Usaidizi wa kina mama , watoto watakapoanza shule, tutakapostaafu.

Hauhitaji mwaliko kabla uanze kuchukua hatua katika kutimiza malengo yako ya haki. Hauhitaji ungojee ruhusa ili uwe mtu uliyefaa kuwa. Hauhitaji ungojee ualikwe kuhudumu Kanisani

Saa zingine tunaweza kupoteza miaka ya maisha yetu tukingoja tuchaguliwe (ona M&M 121:34–36). Lakini hicho ni kigezo cha uongo. Tayari umechaguliwa!

Wakati mwingine maishani mwangu nimekosa usingizi nikiwa ninakumbana na maswala, masumbuko, ama masikitiko ya kibinafsi. Lakini bila kujali kiwango cha hofu, daima mimi hutiwa moyo na wazo hili: asubuhi jua litapambazuka.

Na kila siku mpya, pambazuko jipya huja — si tu kwa dunia lakini kwetu pia. Na pamoja na siku mpya, huja mwanzo mpya — fursa ya kuanza upya.

Lakini, Je Tukishindwa?

Wakati mwengine kile kinachotuzuia ni hofu. Tunaweza kuogopa kwamba hatutafanikiwa, kwamba tutafanikiwa, kwamba huenda tutaaibika, kwamba ufanisi huenda ukatubadilisha, ama kwamba huenda ukabadilisha watu tunaowapenda.

Na basi tunangoja. Ama kukata tamaa.

Jambo lingine tunalohitaji kukumbuka tunapoweka malengo ni hili: Huenda hakika tukashindwa — angalau kwa muda mfupi. Lakini badala ya kukata tamaa, tunaweza kuwezeshwa kwa sababu ufahamu huu unao ondoa shinikizo la kuwa kamili kabisa sasa hivi. Unakubali kutoka mwanzo kwamba wakati mmoja ama mwingine, huenda tukawa na mapungufu. Kujua hivi mwanzoni kunaondoa mshangao na kuvujika moyo kwa ajili ya kushindwa.

Tunapoyafuata malengo yetu kwa njia hii, kushindwa hakufai kutuzuia. Kumbuka, hata tukishindwa kufika tunapotaka kufika mara moja, tutakuwa tumefanya maendeleo kwenye njia itakayoelekeza huko.

Na hiyo ni muhimu — ina maana sana.

Hata ingawa tunaweza kushindwa kufikia mstari wetu wa kumaliza, kuendelea na safari tu kutatufanya tuwe bora zaidi kuliko tulivyokuwa awali.

Wakati Bora wa Kuanza ni Sasa

Msemo wa kale unasema, “Wakati bora wa kupanda mti ni miaka 20 iliyopita. Wakati wa pili-bora ni sasa.”

Kuna kitu cha ajabu na cha matumaini kuhusu neno sasa. Kuna jambo la kuwezesha kuhusu ukweli kuwa tukichagua kuamua sasa, tunaweza kuendelea mbele mara moja.

Sasa ndio wakati bora wa kuanza kuwa mtu ambaye hatimaye tunataka tuwe — si tu miaka 20 kutoka sasa lakini pia milele na milele.

Kufundisha kutoka kwa Ujumbe huu

Rais Uchtdorf alieleza kwamba tunaposhindwa kufikia malengo yetu, “tunaweza kuwezeshwa. Hata ingawa tunaweza kushindwa kufikia mstari wetu wa kumaliza, kuendelea na safari tu kutatufanya tuwe bora zaidi kuliko tulivyokuwa awali. Uliza wanafamilia washiriki matukio ambako walijifunza zaidi kutoka kwa mfanyiko badala ya walichojifunza kutoka kwa matokeo, kama vile kuhitimu kutoka shuleni ama kupokea tuzo.