Ujumbe wa Mwalimu Mtembelezi, Januari 2014
Wito Mtakatifu wa Yesu Kristo: Mfano
Soma mambo haya kwa maombi na utafute kujua kile cha kushiriki. Kuelewa maisha na wito wa Mwokozi kutaongezaje imani yako Kwake na kubariki wale unaowalinda kupitia mafunzo ya utembelezi? Kwa taarifa zaidi, nenda kwenye www.reliefsociety.lds.org.
Tunapoelewa kwamba Yesu Kristo ni mfano wetu katika vitu vyote, tunaweza kuongeza hamu yetu ya kumfuata Yeye. Maandiko yamejaa himizo kwetu kufuata katika nyayo za Kristo. Kwa Wanefi Kristo alisema, “Kwani vitendo ambavyo mmeniona nikifanya, hivyo pia mtafanya” (3 Nefi 27:21). Kwake Tomaso, Yesu alisema, “Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima: mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi (Yohana 14:6).
Siku za leo viongozi wetu wanatukumbusha kumweka Mwokozi kama mfano wetu. Linda K. Burton, rais mkuu wa Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama, alisema, “Wakati kila mmoja wetu ana mafundisho ya Upatanisho yameandikwa ndani katika mioyo yetu, basi tutaanza kuwa aina ya watu ambao Bwana anataka tuwe.”1
Rais Thomas S. Monson alisema, “Bwana na Mwokozi Wetu, Yesu Kristo, ndiye Mfano wetu na nguvu yetu.”2
Tuazimie kusongea karibu na Yesu Kristo, kutii amri Zake, na kujitahidi kurudi kwa Baba yetu wa Mbinguni.
Kutoka kwenye Maandiko
Kutoka kwenye Historia Yetu
“Alionyesha njia na kuongoza njiani,” aliandika Eliza R. Snow, rais mkuu wa pili wa Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama, kuhusu huduma ya duniani ya Yesu Kristo.3 Alihudumia watu binafsi — mmoja baada ya mwingine. Alifundisha kwamba tunapaswa tuwaache wale tisini na tisa ili kuokoa yule moja aliyepotea (ona Luka 15:3–7). Aliponya na kufundisha watu binafsi, hata akichukua muda kwa ajili ya kila mtu katika umati wa watu 2,500 (ona 3 Nefi 11:13–15; 17:25).
Kuhusu wanawake wa Siku za Mwisho, Rais Dieter F. Uchtdorf, Mshauri wa Pili katika Urais wa Kwanza, alisema: “Ninyi akina dada wema hutoa huduma ya fadhila kwa wengine kwa sababu zinazoshinda tamaa ya kijinufaisha kibinafsi. Katika mambo haya nyinyi huiga Mwokozi. Mawazo Yake daima yalielekezwa kuwasaidia wengine.”4
© 2014 by Intellectual Reserve, Inc. Haki zote zimehifadhiwa. Imechapishwa USA. Kiingereza kiliidhinishwa: 6/13. Tafsiri iliidhinishwa: 6/13. Tafsiri ya Visiting Teaching Message, January 2014. Swahili. 10861 743