2014
Jibu la Ombi Lake
Machi 2014


Vijana

Jibu la Ombi Lake

Mwandishi anaishi Gauteng, Afrika Kusini.

Usiku mmoja rafiki wa imani nyingine alinitembelea. Kwa kawaida mimi hujifunza maandiko peke yangu, na nilikuwa nimeyatoa ili kuyasoma usiku huo. Nilishawishiwa kumwalika tuungane katika mafunzo yangu ya maandiko, lakini nilikuwa na hofu na badala yake kuanza kusoma peke yangu. Nilijua kwamba nilikuwa nimepuuza ushawishi wa Roho. Baada ya dakika chache niliuliza kwa tahadhari, “Je, ungependa kusoma maandiko pamoja nami?” Bila ya kusita rafiki yangu alijibu, “Ndiyo.”

Kisha tukasoma kutoka kwa Kitabu cha Mormoni. Aliniuliza baadhi ya maswali, na ningehisi Roho akiniongoza nilipokuwa nikijibu. Nilitoa ushuhuda wangu wa ukweli wa Kitabu cha Mormoni. Baada ya kufanya hivi, aliniambia, “Nimekuwa nikilia na kuhofia siku nzima. Nilikuwa nimetoka tu kumwomba Mungu kwa ajili ya usaidizi ndipo uliniomba nisome nawe maandiko. Ninajihisi vyema zaidi sasa. Asante.”

Bwana alikuwa amenitumia kama chombo kujibu ombi na kuhudumia mmoja wa watoto Wake walio na hitaji. Najua kwamba ushawishi ni maelekezo tukufu kutoka kwa Baba mwenye hekima, na mtukufu. Tunapoweka kando hofu zetu, tunamruhusu Yeye aonyeshe nguvu Yake kupitia kwa utiifu wetu.

Chapisha