2014
Misheni Tukufu ya Yesu Kristo: Nuru ya Ulimwengu
Machi 2014


Ujumbe wa Mwalimu Mtembelezi, Machi 2014

Misheni Tukufu ya Yesu Kristo: Nuru ya Ulimwengu

Soma mambo haya kwa maombi na utafute kujua kile cha kushiriki. Kuelewa maisha na wito wa Mwokozi kutaongezaje imani yako Kwake na kubariki wale unaowalinda kupitia mafunzo ya utembelezi? Kwa maelezo zaidi, nenda kwenyewww.reliefsociety.lds.org.

Imani • Familia • Usaidizi

Tunapokuja kuelewa kwamba Yesu Kristo ni Nuru ya Ulimwengu, tutaongeza imani yetu Kwake na kuwa nuru kwa wengine. Kristo alishuhudia juu ya jukumu Lake kama “nuru ya kweli imwangazayo kila mtu [mwanaume na mwanamke] ajaye ulimwenguni” (M&M 93:2) na akauliza kwamba “tuinue juu nuru [Yake] kwamba iangaze juu ya dunia” (3 Nephi 18:24).

Manabii wetu wameshuhudia pia juu ya Nuru ya Kristo. Rais Henry B. Eyring, Mshauri wa Kwanza katika Urais wa Kwanza, alisema: “Kila wakati unachagua kujaribu kuishi zaidi kama Mwokozi, ushuhuda wako utaimarishwa. Utakuja kwa muda kujijulia mwenyewe kwamba Yeye ndiye Nuru ya Ulimwengu. Utaangaza kwa wengine Nuru ya Kristo maishani mwako.1

Mzee Quentin L. Cook wa Jamii ya Mitume Kumi na Wawili alisema kuhusu kuwa kwetu nuru kwa Ulimwengu: “Tunahitaji kulinda familia zetu na kuwa kwenye mstari wa mbele pamoja na watu wote wenye nia nzuri katika kufanya kila kitu tunachoweza ili kuhifadhi nuru, tumaini, na maadili katika jamii zetu.”2

Kutoka kwenye Maandiko

Yohana 8:12; Mafundisho na Maagano 50:24; 115:5

Kutoka kwenye Historia Yetu

Wanawake Watakatifu wa Siku za Mwisho wanaendelea kuinua nuru yao.

Kwenye ghorofa ya 80 ya jumba refu kule Hong Kong, China, dada mseja mwenye ulemavu — Mtakatifu wa Siku za Mwisho pekee katika familia yake — aliitengeneza nyumba ambayo ilikuwa bandari ambapo yeye na wageni wangeweza kuhisi ushawishi wa Roho. Aliweka maandiko yake, vitabu vya kiada vya Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama, na kitabu chake cha nyimbo karibu. Alisafiri kwenda hekaluni kufanya maagizo kwa ajili ya mababu zake.3

Kule Brazil mama mwenye haki aliwalea watoto wake katika nuru ya injili. Nyimbo za Msingi ziliimbwa katika nyumba yake ya matofali mekundu, na picha kutoka kwa Liahona ya hekalu, manabii wa Mungu, na Mwokozi zilifunika kuta. Yeye na mumewe walijitolea ili kuunganishwa katika hekalu ili watoto wao waweze kuzaliwa katika agano. Maombi yake ya kila mara yalikuwa kwamba Bwana angemsaidia kuwalea watoto wake katika nuru, ukweli, na nguvu ya injili.4

Muhtasari

  1. Henry B. Eyring, “A Living Testimony,” Ensign ama Liahona, Mei 2011, 128.

  2. Quentin L. Cook, “Let There Be Light!” Ensign ama Liahona, Nov. 2010, 30.

  3. Ona Daughters in My Kingdom: The History and Work of Relief Society (2011), 163–64.

  4. Ona Daughters in My Kingdom, 164.

Chapisha