2014
Wito Mtakatifu wa Yesu Kristo: Mtetezi
Julai 2014


Ujumbe wa Mwalimu Mtembelezi, Julai 2014

Wito Mtakatifu wa Yesu Kristo: Mtetezi

Kwa maombi soma mambo haya na utafute kujua kile cha kushiriki. Kuelewa maisha na ujumbe wa Mwokozi kutaongezaje imani yako Kwake na kubariki wale unaowaongoza kupitia ualimu tembelezi? Kwa taarifa zaidi, nenda kwenye reliefsociety.lds.org.

Imani, Familia, Usaidizi

Yesu Kristo ndiye Mtetezi wetu kwa Baba. Neno mtetezi lina mizizi ya Kilatini “anayemtetea mwingine.”1 Mwokozi anatutetea, akitumia ufahamu, haki, na rehema. Kujua haya kunaweza kutujaza na upendo na shukrani kwa ajili ya Upatanisho Wake.

“Msikilizeni [Yesu Kristo] aliye mwombezi kwa Baba, anayetetea mambo yetu mbele zake—

“Akisema: Baba, tazama mateso na kifo chake yeye ambaye hakutenda dhambi, ambaye ulipendezwa naye; tazama damu ya mwanao iliyomwagika; damu yake yeye ambaye ulimtoa ili upate kutukuzwa;

“Kwa hiyo, Baba, wasamehe hawa ndugu zangu ambao wanaamini juu ya neno langu, ili waweze kuja kwangu na kupata uzima usio na mwisho” (M&M 45:3–5).

Kwa Kristo kama Mtetezi wetu, Mzee D. Todd Christofferson wa Jamii ya Mitume Kumi na Wawili alisema: “Ni ya umuhimu mkubwa kwangu, kwamba ningeweza kwa muda wowote na katika hali yoyote kukaribia kupitia maombi kiti cha neema, kwamba Baba wa Mbinguni atasikia maombi yangu, kwamba Mtetezi wangu, ambaye hakutenda dhambi yoyote, ambaye damu yake ilimwagwa, atanitetea kesi yangu.”2

Kutoka kwenye Maandiko

Mosia 15:8–9; Moroni 7:28; Mafundisho na Maagano 29:5; 110:4

Kutoka kwa Historia Yetu

Katika historia yote ya Kanisa la Bwana, wafuasi wa kike wa Yesu Kristo wamefuata mfano Wake. Esta alikuwa mtetezi mwaminifu na mjasiri. Binamu yake Mordekai alimtumia nakala ya andiko la mbiu ya mfalme kwamba Wayahudi walipaswa kuangamizwa, na alimuagiza “kumsihi [mfalme] na kuwaombea watu wake.” Aliongeza: “Walakini ni nani ajuae kama wewe hukuujia ufalme kwa ajili ya wakati kama huo?” (Esta 4:8, 14.)

Licha ya hatari ya kuwa mtetezi wa watu wake, Esta alikubali: “Kisha nitaingia kwa mfalme, kinyume cha sheria; nami nikiangamia, na niangamie” (Esta 4:16).

Esta kisha alizungumza kwa unyenyekevu kwa mfalme na “akaanguka miguuni pake, akamsihi kwa machozi kuzitengua barua kuwaangamiza Wayahudi.” Aliongeza, “Niwezeje kuyaona mabaya yatakayowajia watu wangu?” (ona Esta 8:3, 5–6). Moyo wa mfalme ulilainika, na akakubali ombi lake.3

Muhtasari

  1. Ona Russell M. Nelson, “Jesus Christ—Our Master and More” (Brigham Young University fireside, Feb. 2, 1992), 4; speeches.byu.edu.

  2. D. Todd Christofferson, “I Know in Whom I Have Trusted,” Ensign, Mei 1993, 83.

  3. Ona pia Daughters in My Kingdom: The History and Work of Relief Society (2011), 180.

Zingatia Haya

Utetezi wa Yesu Kristo unawezaje kutuvutia kuonyesha huruma na msamaha kwa wengine?

Chapisha