Ujumbe wa Mwalimu Mtembelezi, Agosti 2014
Wito Mtakatifu wa Yesu Kristo: Masiya
Kwa maombi soma mambo haya na utafute kujua kile cha kushiriki. Kuelewa maisha na majukumu ya Mwokozi kutaongezaje imani yako Kwake na kubariki wale unaowaongoza kupitia ualimu tembelezi? Kwa maelezo zaidi, nenda kwenye reliefsociety.lds.org.
Maandiko yanafundisha kwamba tunaweza kuishi katika uwepo wa Mungu “kupitia fadhila, na rehema, na neema za Masiya Mtakatifu” (2 Nefi 2:8). Masiya ni “neno la Kiaramu na Kiyahudi linalomaanisha ‘aliye takaswa.’ Katika Agano Jipya Yesu anaitwa Kristo, ambayo kwa Kigiriki ni kisawe cha Masiya. Ina maana Mtume aliyetakaswa, Kuhani, Mfalme, na Mkombozi.1
Mzee Jeffrey R. Holland wa Jamii ya Mitume Kumi na Wawili alishuhudia: “Ninajua [Yesu Kristo] ndiye Yule Mtakatifu wa Israeli, Masiya. ambaye siku moja atakuja tena katika utukufu wa mwisho, kutawala duniani kama Bwana wa mabwana na Mfalme wa wafalme. Najua kwamba hakuna jina lingine lililotolewa chini ya mbinguni ambapo mwanaume [ama mwanamke] anaweza kuokolewa.2
“[Yesu Kristo] ndiye Mwokozi na Mkombozi wa dunia,” alisema Rais Dieter F. Uchtdorf, Mshauri wa Pili katika Urais wa Kwanza. “Ndiye Masiya aliyeahidiwa. Aliishi maisha makamilifu na alilipia dhambi zetu. Daima atakuwa kando yetu. Atapigana vita vyetu. Ndiye tumaini letu; Ndiye ukombozi wetu; Ndiye njia.”3
Maandiko ya Ziada
Kutoka kwenye Maandiko
Wanafunzi wa kike wa Kristo wamekuwa mashahidi wa jukumu Lake kama Masiya. Mariamu Magdalene alikuwa mwanafunzi wa Yesu Kristo. Alikuwa wa kwanza kuona “jiwe limeondolewa kaburini” asubuhi ya Ufufuo wa Kristo. Alisimama “nje ya kaburi analia” baada ya kugundua kwamba mwili Wake haukuwa kaburini.
Kisha “akageuka nyuma, akamwona Yesu amesimama, asijue ya kuwa ni Yesu.
“Yesu akamwambia, Mama, unalilia nini? Unamtafuta nani? Naye, huku akidhani ya kuwa ni mtunza bustani, akamwambia, Bwana, ikiwa umemchukua wewe, uniambie ulipomweka, nami nitamwondoa.
“Yesu akamwambia, Mariamu. Yeye akageuka, akamwambia, Raboni; yaani, Mwalimu wangu.” Mariamu aligundua kwamba Yeye hakuwa mtunza bustani lakini Yesu Kristo, Masiya (ona Yohana 20:1–17.)
© 2014 by Intellectual Reserve, Inc. Haki zote zimehifadhiwa. Imechapishwa Marekani. Kiingereza kiliidhinishwa: 6/14. Tafsiri iliidhinishwa: 6/14. Tafsiri ya Visiting Teaching Message, August 2014. Swahili. 10868 743