2015
Ushauri kwa ajili ya Chaguo Ngumu
Januari 2015


Vijana

Ushauri kwa ajili ya Uamuzi Mgumu

Rais Henry B. Eyring, Mshauri wa Kwanza katika Urais wa Kwanza, alisimulia kuhusu wakati alifuata ushauri wa kinabii. Wakati wa mkutano mkuu mmoja, Rais Ezra Taft Benson (1899–1994) aliwahimiza washiriki waepuke madeni —hasa deni la kununua nyumba.

Rais Eyring alisema: “Nilimgeukia mke wangu baada ya mkutano na kumuuliza, ‘Je, unafikiria kuna njia yoyote tunaweza kufanya hivyo?’ Mwanzoni hatungeweza.” Lakini jioni hiyo alifikiria kuhusu nyumba aliyokuwa amejaribu kuuza bila kufanikiwa kwa miaka mingi. “Tulimuamini Mungu na ujumbe wa mtumishi Wake, [basi] tulipiga simu. Nilisikia jibu ambalo hadi leo linaimarisha imani yangu katika Mungu na watumishi Wake.” Siku hiyo hiyo mtu alikuwa ameweka toleo la ununuzi kwenye nyumba ya akina Eyring ya kiasi zaidi ya deni la nyumba yao. Akina Erying punde wakawa huru wa deni (ona “Trust in God, Then Go and Do,” Liahona, Nov. 2010, 72–73).

Huenda usiwe na deni la nyumba la kulipa, lakini ushauri wa unabii unaweza kukuongoza hapa na sasa kupita maamuzi magumu kuhusu kazi, elimu, misheni, na kuchumbiana. Jadiliana na familia yako ama wenzako kuhusu jinsi unaweza kumfuata nabii wakati unataka kufanya maamuzi.

Chapisha