2015
Sifa za Yesu Kristo: Mwana Mtiifu
Januari 2015


Ujumbe wa Mwalimu Mtembelezi, Januari 2015

Sifa za Yesu Kristo: Mwana Mtiifu

Kwa maombi jifunze nyenzo hii na tafuta kujua nini cha kushiriki. Kuelewa maisha na wajibu wa Mwokozi kunawezaje ongeza imani yako Kwake na kubariki wale unaowaongoza kupitia ualimu tembelezi? Kwa taarifa zaidi, nenda kwenye reliefsociety.lds.org.

Imani, Familia, Usaidizi

Kufuata mfano wa Yesu Kristo wa utiifu kunaongeza imani yetu Kwake. “Je, inashangaza,” alisema Mzee Jeffrey R. Holland wa Jamii ya Mitume Kumi na Wawili, “kwamba Kristo anachagua kwanza kabisa kujieleza juu ya uhusiano wake na baba yake — kwamba alimpenda na kumtii na kujiwasilisha kwake kama mwana mwaminifu aliyekuwako? “Utiifu ni sheria ya kwanza ya mbinguni.”1

Maandiko yanafundisha “na kama tunapata baraka yoyote kutoka kwa Mungu, ni kutokana na utii kwa sheria ile ambayo juu yake hutoka” (M&M 130:21). Kukua kwetu kiroho hufanyika tunapomkaribia Mungu kupitia utiifu na kualika nguvu ya Upatanisho wa Mwokozi katika maisha yetu.

“Tunapotembea katika utiifu wa kanuni na amri za injili ya Yesu Kristo,” alisema Mzee D. Todd Christofferson wa Jamii ya Mitume Kumi na Wawili, “tunafurahia mtiririko unaoendelea wa baraka zilizoahidiwa na Mungu katika agano Lake nasi. Baraka hizo hutoa nyenzo tunazohitaji kutenda badala ya kutendewa tu tunapopitia maisha. Utiifu unatupa nguvu zaidi juu ya maisha yetu, uwezo zaidi wa kuja na kwenda, kufanya kazi na kubuni.”2

Maandiko ya Ziada

Luka 22:41–46; Mafundisho na Maagano 82:10; 93:28

Kutoka katika Maandiko

“Je, nguvu ya kiroho inayotokana na utiifu wa kila mara wa amri inaweza kupewa mtu mwingine?” aliuliza Mzee David A. Bednar wa Jamii ya Mitume Kumi na Wawili. “Jibu wazi ni hapana.”3

Fumbo la wanawali kumi ni mfano wa kanuni hii. Ingawa wanawali wote walichukua taa zao ili “kumlaki bwana harusi” watano tu ndio waliokuwa wenye busara na walichukua mafuta katika taa zao. Wale watano wengine walikuwa wapumbavu kwa sababu “hawakutwaa mafuta pamoja nao.”

Kisha pakawa na kelele usiku wa manane: “Haya, bwana harusi anakuja, tokeni mwende kumlaki.” Wanawali wote walizitengeneza taa zao, lakini wanawali wapumbavu hawakuwa na mafuta. Waliwaambia wanawali wenye busara, “Tupeni mafuta yenu kidogo; maana taa zetu zinazimika.”

Wanawali wenye busara walijibu, “Sivyo; hayatatutosha sisi na ninyi: afadhali shikeni njia mkajinunulie wenyewe.” Na wakati wanawali wapumbavu walikuwa wameenda, bwana harusi alikuja na wanawali wenye busara walienda naye na “mlango ukafungwa”

(Mathayo 25:1–13).

Muhtasari

  1. Jeffrey R. Holland, “The Will of the Father in All Things” (Brigham Young University devotional, Jan. 17, 1989), 4, speeches.byu.edu.

  2. D. Todd Christofferson, “The Power of Covenants,” Liahona, Mei 2009, 21.

  3. David A. Bednar, “Converted unto the Lord,” Liahona, Nov. 2012, 109.

Zingatia Haya

Ni ipi baadhi ya mifano ya utiifu katika maandiko?