2015
Kuweka Kumbu kumbu
Julai 2015


Vijana

Kuweka Kumbu-kumbu

Rais Uchtdorf analinganisha siku zetu na nyakati za waanzilishi. Ingawa huenda hukuvuka nyika, unafanana na waanzilishi zaidi ya unavyofikiria! Wewe pia unaweza kuonyesha huruma, bidii, na tumaini. Na kama vile tunavyojua kwamba waanzilishi walionyesha sifa hizi kwa sababu ya kumbukumbu walizoweka, ukoo wako unaweza kujua kupitia shajara yako pia.

Chukua dakika chache kuandika kidogo juu yako wewe mwenyewe katika shajara yako. Unaweza kuandika kuhusu vitu vya kiroho, kama vile jinsi ulivyopata ushuhuda wako ama ulivyoshinda changamoto kwa usaidizi wa Baba wa Mbinguni. Unaweza pia kuwasaidia vitukuu wako (ambao huenda wakasoma shajara yako siku moja!) kujua jinsi maisha yako ya kila siku yalivyokuwa. Ni miradi gani unayofanya shuleni? Chumba chako kinafananaje? Ni kumbu-kumbu gani ya familia yako unayoipenda zaidi?

Unapoanza kuandika kidogo kila siku, hutaweza tu kuona vyema zaidi jinsi Baba wa Mbinguni anavyokusaidia katika maisha yako ya kila siku, kama tu vile alivyowaongoza waanzilishi, lakini pia utakuwa unaacha urithi kwa ukoo wako ujao.

Chapisha