2015
Sifa za Kiungu za Yesu Kristo: Mwenye Kusamehe na Kurehemu
Julai 2015


Ujumbe wa Mwalimu MTEMBELEAJI, Julai 2015

Sifa za Kiungu za Yesu Kristo: Mwenye Kusamehe na Kurehemu

Kwa maombi jifunze maneno haya na utafute kujua kitu cha kuelezea. Je kuelewa maisha na nafasi za Mwokozi kunawezaje kuongeza imani yako Kwake na kuwabariki wale unaowaongoza kupitia ualimu wa kutembelea? Kwa taarifa zaidi, nenda reliefsociety.lds.org

Imani, Familia, Usaidizi

Kuelewa kwamba Yesu Kristo amekuwa mwenye kutusamehe na kuturehemu kunaweza kutusaidia kusamehe na kurehemu wengine. “Yesu Kristo ni Kielelezo Chetu,” alisema Rais Thomas S. Monson. Maisha yake ni urithi wa upendo. Wagonjwa aliwaponya; waliokandamizwa aliwainua; mwenye dhambi alimwokoa. Mwishoni kundi la watu wenye hasira liliangamiza maisha Yake. Na bado kuna mwangwi kutoka kilima cha Golgotha wa maneno: “Baba, uwasamehe, kwa kuwa hawajui watendalo.” 4— maonyesho ya kipeo katika maisha ya duniani ya huruma na upendo.1

Tukiwasamehe wengine makosa yao, Baba yetu wa Mbinguni atatusamehe sisi pia. Yesu anatuamuru “muweni na huruma, kama Baba yenu alivyo na huruma” (Luka 6:36). “Msamaha wa dhambi zetu huja na masharti,” alisema Rais Dieter F. Uchtdorf, Mshauri wa Pili katika Urais wa Kwanza. “Lazima tutubu. Je, si sisi sote, wakati mmoja, au mwingine, kwa unyenyekevu tumekuja katika kiti cha enzi, na kuomba neema? Je, hatujatamani rehema kwa uwezo wote wa mioyo yetu —kusamehewa kwa makosa tuliyofanya na dhambi tulizotenda? Kubali Upatanisho wa Kristo kubadili na kuponya roho yako. Pendaneni Semeheaneni.”2

Maandiko ya Ziada

Mathayo 6:14–15; Luka 6:36–37; Alma 34:14–16

Kutoka katika Maandiko

“Tunapaswa tusamehe hata kama vile sisi tunavyosamehewa,” alisema Mzee Jeffrey R. Holland wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili.3 Hadithi ya mwana mpotevu inatuonyesha pande zote mbili za msamaha: mwana mmoja anasamehewa na mwana mwingine anaona ugumu wa kusamehe.

Mwana mdogo alichukua urithi wake, akautumia kwa haraka, na wakati njaa ilipokuja, alifanya kazi akiwalisha nguruwe. Maandiko yanasema “alipozingatia moyoni mwake,” alirudi nyumbani na kumwambia babake hakustahili kuwa mwana wake. Lakini babake alimsamehe na kuchinja ndama aliyenona kwa ajili ya karamu. Mwana mkubwa alirudi kutoka kufanya kazi katika shamba na akakasirika. Alimkumbusha babake kwamba alikuwa amehudumu miaka mingi, hakuwahi kukiuka amri, lakini “hujanipa mimi mwana-mbuzi, nifanye furaha na rafiki zangu.” Baba alijibu, “Mwanangu, wewe u pamoja nami siku-zote, na vyote nilivyo navyo ni vyako. Kufanya furaha na shangwe ilipaswa, kwa kuwa huyu ndugu yako alikuwa amekufa, naye amefufuka; alikuwa amepotea, naye ameonekana” (ona Luka 15:11–32).

Muhtasari

  1. Thomas S. Monson, Upendo—Kiini cha Injili, Liahona, Mei 2014, 91.

  2. Dieter F. Uchtdorf, “The Merciful Obtain Mercy,” Liahona, Mei 2012, 70, 75, 77; himizo katika nakala halisi.

  3. Jeffrey R. Holland, “The Peaceable Things of the Kingdom,” Ensign, Nov. 1996, 83.

Zingatia Hili

Kusamehe kunawezaje kumnufaisha anayesamehe?