2015
Sifa za Utukufu za Yesu Kristo: Kujawa na Hisani na Upendo
Oktoba 2015


Ujumbe wa Mwalimu Mtembelezi, Oktoba 2015

Sifa za Utukufu za Yesu Kristo: Kujawa na Hisani na Upendo

Kwa maombi jifunze maneno haya na utafute kujua kitu cha kushiriki. Kuelewa sifa za utukufu za Mwokozi kunawezaje kuongeza imani yako Kwake na kuwabariki wale unaowachunga kwa njia ya ualimu wa kutembelea? Kwa taarifa zaidi, nenda kwenye www.reliefsociety.lds.org.

Imani, Familia, Usaidizi

Mwongozo wa Maandiko unaelezea hisani kama aina ya upendo wa juu sana, wa uadilifu, wa nguvu sana (Hisani). Hisani ni upendo msafi wa Kristo. Tunapojifunza juu ya Yesu Kristo na kujitahidi kuwa kama Yeye, tutaanza kuhisi upendo Wake halisi katika maisha yetu na kusukumwa kupenda na kuwatumikia wengine kama vile Yeye angetumikia. Hisani ni kuwa na uvumulivu na mtu ambaye amekuangusha, Rais Thomas S Monson alisema “Ni kupinga mvuto wa kukasirishwa kwa urahisi. Ni kukubali udhaifu na upungufu. Ni kuwakubali watu kama hakika walivyo.” Ni kuangalia zaidi ya sura ya kimwili hata kwa sifa ambazo hazitafifia kwa wakati. Ni kupinga mvuto wa kuainisha wengine.1

Katika Kitabu cha Mormoni, tunajifunza ukweli mkuu kwamba “Tuombe kwa Baba kwa nguvu za zote za moyo kwamba tujazwe upendo huu, ambao ametoa kwa wote ambao ni wafuasi wa kweli wa Mwana wake, Yesu Kristo; ili muwe wana wa Mungu; kwamba wakati atakapoonekana tutakuwa kama yeye, kwani tutamwona vile alivyo; ili tuwe na tumaini hili; ili tutakaswe hata vile alivyo mtakatifu” (Moroni 7:48).

Maandiko ya Ziada

Yohana 13:34–35; 1 Wakorintho 13:1–13; 1 Nefi 11:21–23; Etheri 12:33–34

Kutoka katika Historia Yetu

Dada ambaye hivi karibuni amekuwa mjane alikuwa na shukrani kwa walimu watembeleaji ambao waliomboleza pamoja naye na kumfariji. Aliandika: “Nilikuwa na haja sana ya mtu ambaye ningemfikia; mtu ambaye angenisikiliza mimi. Na walinisikiliza. Walinifariji Walilia nami Na walinikumbatia [na] walinisaidia kutoka kwenye dhiki kuu na mateso ya miezi ya kwanza ya upweke.”

Mwanamke mwingine alielezea hisia zake wakati alipokuwa mpokeaji wa hisani ya kweli kutoka kwa mwalimu mtembeleaji: “Mimi nilijua kwamba nilikuwa zaidi ya nambari kwenye kitabu cha kumbukumbu yake ya kumtembelea. Nilijua kwamba alinijali.”2

Kama kina dada hawa, Watakatifu wa Siku za Mwisho kote ulimwenguni wanaweza kushuhudia ukweli wa kauli hii ya Rais Boyd K Packer (1924-2015), Rais wa Akidi ya wale Mitume Kumi na Wawili: “Inafariji jinsi gani kujua kwamba haijalishi pale [familia inaweza] kwenda, familia ya Kanisa inawangojea. Toka siku watakayowasili, mme atakuwa katika akidi ya ukuhani naye atakuwa katika Muungano wa Usaidizi wa kina mama.”3

Muhtasari

  1. Thomas S. Monson, Hisani Kamwe Haipungui Liahona Nov. 2010, 124.

  2. Daughters in My Kingdom: The History and Work of Relief Society (2011), -120.

  3. Daughters in My Kingdom, 87.

Zingatia Hili

Je! Ni kwa jinsi gani Kristo ni mfano wetu mkamilifu wa upendo na hisani?