2015
Fanya Mwenge Wako Uangaze zaidi
Oktoba 2015


Watoto

Fanya Mwenge Wako Uangaze zaidi

Hapo kale katika Ugiriki, kulikuwa na mbio ambapo wakimbiaji walishikilia mwenge unaowaka. Mtu yeyote ambaye angekimbia mbio yote na mwenge ukiwa bado umewaka angekuwa mshindi. Rais Uchtdorf anasema maisha ni kama mbio hiyo. Mwenge tunaoshikilia ni Nuru ya Kristo. Tunapojaribu kuwa kama Yesu Kristo, tunafanya mienge yetu kuwaka kwa uangavu.

Je! vitu gani unaweza kufanya ili kuwa kama Yesu na kufanya mwenge wako kuwaka kwa uangavu. Chagua kutoka katika orodha iliyopo hapa chini:

  • Tabasamu au mwamkie mtu anayeonekana kuwa mpweke.

  • Mkasirikie mtu fulani

  • Tunza mwili wako

  • Mdhihaki kaka au dada yako

  • Mtii nabii

  • Kufa moyo unapofanya kosa

  • Msaidie mtu fulani

Chapisha