Ujumbe wa Urais wa Kwanza, Oktoba 2015
Maliza na Mwenge Wako Ukiwa Bado Unawaka
Katika Ugiriki ya kale, wakimbiaji walimaliza mbio za kupokezana zilizoitwa lampadedomia.1 Katika mbio hizi, wakimbiaji walishikilia mwenge katika mkono wao na kumpokeza mkimbiaji anayefutia mpaka mshiriki wa mwisho wa timu anapovuka mstari wa kumaliza.
Tuzo lilikuwa halitolewi kwa timu ambayo ilikuwa na mbio sana—lilitolewa kwa timu ya kwanza kufika kwenye mstari wa kumaliza ikiwa bado mwenge unawaka.
Kuna somo muhimu sana hapa, moja ambalo lilifunzwa na manabii wa kale na kisasa: hali ilikuwa ni muhimu kuanza mbio, vile vile ilikuwa muhimu sana kwamba tumalize tukiwa na mwenge wetu bado unawaka.
Sulemani Alianza kwa Uthabiti
Mfalme mkuu Sulemani ni mfano wa mtu ambaye alianza kwa uthabiti. Wakati alipokuwa kijana, naye akampenda Bwana, akienda katika amri za Daudi babaye (1 Wafalme 3:3). Mungu alipendezwa naye na akasema, Omba utakalo nikupe (1 Wafalme 3:5).
Badala ya kuomba utajiri au maisha marefu, “Sulemani aliomba moyo wa adili niwahukumu watu wako, ili niweze kupambanua mema na mabaya” (1 Wafalme 3:9).
Hili lilimpendeza Bwana sana kwamba Yeye alimbariki Sulemani siyo tu na hekima bali pia na mali isiyo na kifani na maisha marefu.
Ingawa Sulemani alikuwa kwa kweli na hekima sana na alifanya mambo mengi makuu, hakumaliza kwa uthabiti. Cha kuhuzunisha, baadaye katika maisha yake, “Sulemani akafanya yaliyo mabaya machoni pa Bwana, wala hakumfuata Bwana kwa utimilifu” (1 Wafalme 11:6).
Kumaliza Mbio Yetu Wenyewe
Je! Ni mara ngapi tumeanza kitu fulani na hatukimalizi? Milo? Mpango wa Mazoezi? Masharti ya kujifunza maandiko kila siku? Maamuzi ya kuwa wanafunzi bora wa Yesu Kristo.
Je! Ni mara ngapi tumefanya maazimio katika mwezi Januari na kuyafuata kwa azimio la ushupavu kwa siku chache, wiki chache, au hata miezi michache tu na kupata kufikia mwezi Oktoba, ule mwale wa sharti letu ni kidogo zaidi ya jivu baridi.
Siku moja nilipata kuona picha ya kuchekesha ya mbwa aliyelala karibu na kipande cha karatasi alichokuwa amekichanachana. Kiliandikwa, Cheti cha Mafunzo ya Utiifu wa Mbwa.
Sisi tuko hivyo wakati mwingine.
Tunakuwa na dhamira njema; tunaanza kwa uthabiti; tunataka kuwa bora tuwezavyo. Lakini mwishowe tunayaacha maazimio yetu yamechanwachanwa,
Ni asili ya binadamu kujikwaa, kushindwa, na wakati mwingine kujitoa kutoka kwenye mbio. Lakini kama wanafunzi wa Yesu Kristo, hatujaweka tu sharti la kuanza mbio bali pia kumaliza–-na kumaliza na mwenge wetu ukiwa bado unawaka kwa uangavu. Mwokozi aliwaahidi wanafunzi Wake, “Yule atakayevumilia hadi mwisho, huyo ataokolewa” (Mathayo 24:13).
Acha mimi nifafanue kile Mwokozi ameahidi katika siku zetu: Kama tutaweka amri na kumaliza na mwenge wetu bado umewaka, tutapata uzima wa milele, ambacho ndicho kipawa kikuu cha vipawa vyote vya Mungu (ona M&M 14:7; ona pia 2 Nefi 31:20).
Nuru Ambayo Kamwe Haizimi
Wakati mwingine baada ya kujikwaa, kushindwa, au hata kukata tamaa, tunakufa moyo na kuamini nuru yetu imezima na mbio yetu tumeipoteza. Lakini mimi nashuhudia kwamba Nuru ya Kristo haiwezi kuzimwa. Inaangaza katika usiku wa kiza na itaangaza tena mioyo yetu kama tu tutaielekeza mioyo yetu Kwake (ona 1 Wafalme 8:58).
Haijalishi ni mara ngapi au tumeanguka vipi, Nuru ya Kristo daima inawaka kwa uangavu. Na hata katika kina cha kiza cha usiku, kama tutasonga mbele Kwake, nuru Yake itameza vivuli na kuwasha nafsi.
Mbio hii ya ufuasi si fupi; ni mbio ya masafa marefu. Kuna tofauti kidogo juu ya kasi tuliyonayo. Hakika, njia pekee tu tunayoweza kupoteza mbio ni kuvunjika moyo au kushindwa.
Almradi tunaendelea kuinuka na kusonga mbele kwa Mwokozi wetu, tutashinda mbio na mienge yetu ikiwa inawaka kwa uangavu.
Kwani mwenge siyo kuhusu sisi au kile tunachofanya.
Ni kuhusu Mwokozi wa ulimwengu.
Na hiyo ni Nuru ambayo kamwe haiwezi kufifia. Ni Nuru ambayo humeza kiza, huponya vidonda vyetu, na uwaka hata miongoni mwa huzuni ya kina na kiza kisichoeleweka.
Ni Nuru inayoshinda uelewa.
Hebu kila mmoja wetu amalize mapito tuliyoyaanza. Na kwa msaada wa Mwokozi na Mkombozi wetu, Yesu Kristo, tutamaliza kwa shangwe na mienge yetu ikiwa bado inawaka.
© 2015 na Intellectual Reserve, Inc. Haki zote zimehifadhiwa. Imechapishwa Marekani. Kiengereza Kiliidhinishwa: 6/15. Tafsiri Iliidhinishwa: 6/15. Tafsiri ya First Presidency Message, Oktober 2015. Swahili. 12590 743