2015
Tia Mafuta Mwenge Wako: Jaribio la Siku 30
Oktoba 2015


Vijana

Tia Mafuta Mwenge Wako: Jaribio la Siku 30

Kwa vijana wa Kanisa mlio na shughuli nyingi maishani, inaweza kuwa rahisi kukwama katika mrudiomrudio wa kawaida, haswa katika vitu vya kiroho. Tunasoma maandiko yetu, tunaomba, na kuabudu kwa njia ile ile karibu kila siku na kisha kushangaa kwa nini tunaonekana kuwa katika mporomoko wa kiroho.

Mojawapo ya njia bora ya kuweka mwenge wako wa kiroho uwe unawaka kwa uangavu ni kuhakikisha unakuwa na uzoefu wa kiroho wa maana. Lakini ni rahisi kusema kuliko kutenda, kwa hiyo hapa kuna mapendekezo ya kuwasaidia mwendelee katika maendeleo ya kiroho: Fikiria juu ya shughuli inayohusiana na injili ambayo kamwe haujaifanya hapo mbeleni (au kamwe hauifanyi) na uweka sharti la kuifanya kila siku kwa mwezi mmoja. Unaweza kuanza kidogo kidogo kwa sababu utaona ni rahisi kugeuza mabadiliko madogo kuwa ya kudumu. Kufanya vitu ambayo vinavyotuondoa kutoka kwa eneo letu la faraja ya kiroho kunaweza kuhitaji imani zaidi na juhudi katika upande wetu, lakini tunapovifanya, tunamwalika Roho Mtakatifu awe pamoja nasi, na tunaonyesha imani kuu katika Baba wa Mbinguni na hamu ya kujongea karibu Naye. Haya ni mawazo machache ya kukuwezesha kuanza a:

  • Weka lengo la kusema sala zako asubuhi na usiku. Jaribu kusali kwa sauti.

  • Amka dakika 15 mapema na usome maandiko yako kabla kwenda shule.

  • Soma hotuba za mkutano mkuu uliopita.

  • Weka andiko kutoka katika Kitabu cha Mormoni kwenye mtandao wa kijamii.

  • Sikiliza nyimbo au muziki wa Kanisa badala ya muziki wa kawaida.