2015
Njia za Kuhudumu Wakati wa Krismasi
Desemba 2015


Vijana

Njia za Kuhudumu Wakati wa Krismasi

Rais Monson huchukua fursa ya kuwatembelea wakongwe na wale walio kwenye vituo vya malezi, hasa wakati wa Krismasi. Ametambua kwamba kuna wale ambao wana furaha kwa sababu wanapata wageni, hali wengine wanatumainia tu wageni ambao hawaji kamwe. Kuna watu wanaosubiria mtu—labda Krismasi hii, wewe unaweza kuwa mtu huyo anayetumainiwa.

Ifuatayo ni orodha ya njia chache tu za kuhakikisha hakuna mtu anajihisi mpweke Krismasi hii. Jisikie huru kufikiria njia zaidi za kuhudumu katika jumuiya yako msimu huu. Kuna mtu anayengojea matembezi yako?

  • Tengeneza kadi za Krismasi za kuwatumia wamisionari na waumini waseja na waumini wakongwe wa kata au tawi lako.

  • Jitolee katika kundi la taasisi ya kijamii lililo mtaani kwako.

  • Gawa nakala za Kitabu cha Mormoni kama zawadi za Krismasi kwa marafiki na majirani zako.

  • Tembelea wakongwe walio katika kata yako ama familia.

  • Tengeneza vitafunwa na uwapelekee majirani zako.

Chapisha