2015
Sifa za Kiungu za Yesu Kristo: Mwenye Huruma na Mkarimu
Desemba 2015


Ujumbe wa Mwalimu Mtembeleaji, Disemba 2015

Sifa za Kiungu za Yesu Kristo: Mwenye Huruma na Mkarimu

Kwa maombi jifunze maneno haya na utafute kujua kitu cha kushiriki. Kuelewa sifa za kiungu za Mwokozi kunawezaje kuongeza imani yako Kwake na kuwabariki wale unaowachunga kwa njia ya ualimu wa kutembelea? Kwa taarifa zaidi, nenda kwenye www.reliefsociety.lds.org.

Katika maandiko, huruma hasa humaanisha “kuteseka pamoja na”. Pia humaanisha “kuonyesha huruma, kusikitikia, rehema kwa mtu mwingine”.1

“Yesu ametupatia mifano mingi ya huruma”, alisema Rais Thomas S Monson. “Mtu mlemavu katika bwawa la Bethseda; mwanamke aliyepatikana na uzinzi; mwanamke kwenye kisima cha Yakobo; bintiye Yairo; Lazaro, kaka ya Mariamu na Martha—kila mmoja anawakilisha mhasiriwa katika barabara ya Yericho. Kila mmoja alihitaji msaada.

“Kwa mtu mwenye ulemavu huko Bethseda,Yesu alisema, ‘Ondoka, ujitwike godoro lako, na uende’. Kwa mwanamke mzinifu ukaja ushauri, ‘Enenda, na husitende dhambi tena’. Kwa yuke aliyekuja kuchota maji, Alimpatia kisima cha maji yalichupua hata uzima wa milele. Kwa bintiye Yairo ikaja amri, ‘Msichana, nakuambia inuka’. Kwa Lazaro aliyekuwa kaburini, “njoo huku nje”.

“Mwokozi daima amenionyesha kiwango kisicho kifani cha huruma … Acheni tufungue milango ya mioyo yetu. kwamba Yeye—mfano hai wa huruma ya kweli—uweze kuingia”.2

Maandiko ya Ziada

Zaburi 145:8; Zekaria 7:9; 1 Petro 3:8; Mosia 15:1, 9; 3 Nefi 17:5–7

Kutoka katika Maandiko

“Mume wangu nami tulipiga magoti kando ya binti yetu wa miaka 17 na kusihi kwa ajili ya uzima wake”, alisema Linda S. Reeves, mshauri wa pili katika Urais Mkuu wa Muungano wa Usaidizi wa kina Mama. “Jibu lilikuwa hapana, lakini. tumekuja kujua kwamba [Mwokozi] hutuhurumia sisi katika huzuni wetu”.3

“Mojawapo ya hadithi nizipendazo kutoka kwa maisha ya Mwokozi ni ile ya Lazaro. Maandiko yanatuambia kwamba ‘Yesu alimpenda Martha, na dada yake [Mariamu], na [kaka yao] Lazaro’”.4 Wakati Lazaro akiwa mgonjwa, taarifa zilitumwa kwa Yesu, lakini wakati aliwalisi Lazaro alikuwa tayari ameshafariki. Mariamu alimkimbilia Yesu, akaanguka miguuni pake, na kulia. Yesu alipomwona Mariamu akilia, “aliugua rohoni, na akalia machozi” (Yohana 11:33, 35).

“Hiyo ndio kazi yetu. Sisi ni sharti tujisikie na tujionee wenyewe na kisha kuwasaidia watoto wote wa Baba wa Mbinguni kuhisi na kuona kwamba Mwokozi amejichukulia juu Yake mwenyewe siyo tu dhambi zetu zote bali pia maumivu na mateso yetu na masumbuko ili kwamba Yeye aweze kujua kile tunachohisi na jinsi ya kutufariji”.5

Muhtasari

  1. Mwongozo wa Maandiko, “Huruma”

  2. Thomas S. Monson, Kipawa cha Huruma, Liahona, Nov. 2007, 4–5, 8.

  3. Linda S. Reeves, “The Lord Has Not Forgotten You,” Liahona, Nov. 2012, 120.

  4. Linda S. Reeves, “The Lord Has Not Forgotten You,” Liahona, Nov. 2012, 118.

  5. Linda S. Reeves, “The Lord Has Not Forgotten You,” Liahona, Nov. 2012, 120.

Zingatia Hili

Ni nani anayeweza kubarikiwa kwa huruma yako?

Chapisha