2017
Tabasamu Inaweza Kuleta Tofauti Kubwa
Januari 2017


Vijana

Tabasamu Laweza Kuleta Tofauti Kubwa

Rais Uchtdorf anaonyesha malengo mawili ambayo tunapaswa kuyashughulikia: kumpenda Mungu na kuwapenda wanadamu wenzetu. Lakini wakati mwingine si rahisi kuwapenda wengine. Katika maisha yako yote, yawezekana kuwa na nyakati ambapo uliona kuwa vigumu kuchangamana na wengine—labda mtu amekuumiza wewe ama wewe umekuwa na wakati mgumu kuwasiliana ama kuelewana na mtu. Katika nyakati hizi, jaribu kukumbuka upendo ambao umesikia kutoka kwa marafiki, familia, Baba wa Mbinguni, na Yesu Kristo. Kumbuka furaha uliyoisikia katika hali hizo na jaribu kufikiria kama kila mmoja angepata nafasi ya kusikia upendo kama huo. Kumbuka kwamba kila mmoja ni binti au mwana wa Mungu na anafaa yote upendo Wake na wako.

Fikiria mtu mahsusi katika maisha yako ambaye imekuwa vigumu kuelewana naye. Wajumuishe katika maombi yako na muombe Baba wa Mbinguni afungue moyo wako kwao. Punde utaanza kuwaona wao jinsi Yeye anavyowaona: kama mmoja wa watoto Wake ambaye anafaa kupendwa.

Baada ya wewe kuomba, fanya kitu chema kwao! Labda uwaalike kwenye shughuli za Mutuali au matembezi pamoja na marafiki zako. Toa msaada katika kazi ya ziada ya nyumbani. Hata sema tu “jambo” na utabasamu. Mambo madogo yanaweza kuleta tofauti kubwa … katika maisha yenu nyote!

Chapisha