Ujumbe wa Ualimu wa Kutembelea, Januari 2017
Madhumuni ya Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama
Kwa maombi jifunze maneno haya na utafute mwongozo wa kiungu ili kujua kitu cha kufundisha.
Madhumuni ya Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama ni “kuwaandaa wanawake kwa ajili ya baraka za uzima wa milele,” alisema Linda K. Burton, Rais Mkuu wa Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama.1 Ni kwa kupitia imani, familia, na usaidizi ambapo tunajihusisha na “sehemu yetu muhimu katika kazi hii”2
Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama “ni kazi ya kimwili na kiroho,” alisema Carole M. Stephens, Mshauri wa Kwanza katika Urais Mkuu wa Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama. “Hiki ndicho wanawake walifanya katika siku za Mwokozi, na hicho ndicho tunaendelea kufanya.”3
Tunapomuona mwanamke Msamaria kisimani, ambaye aliacha mtungi wake wa maji na kukimbia kuwaambia wengine kwamba Yesu alikuwa ni nabii (ona Yohana 4:6–42), ama Fibi, ambaye kwa furaha aliwahudumia wengine katika maisha yake yote (ona Warumi 16:1–2), tunaona mifano ya wanawake katika siku za Mwokozi ambao walichukua sehemu hai katika kumwendea Kristo. Ni Yeye ambaye hufungua njia yetu hata kuingia katika uzima wa milele (ona Yohana 3:16).
Tunapowatazama dada zetu watangulizi katika Nauvoo, Illinois, ambao walikusanyika katika nyumba ya Sarah Kimball katika mwaka 1842 ili kuanzisha kikundi chao wenyewe, tunaona mpango wa Mungu wa kuzaa Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama na ukiwa katika uwiano na ukuhani. Baada ya Eliza R. Snow kuandika katiba, Nabii Joseph Smith aliihakiki. Akagundua kwamba Kanisa halikuwa limeundwawa kikamilifu hadi wale wanawake walipokuwa wamejipanga. Alisema kwamba Bwana amekubali matoleo yao lakini kuwa palikuwa na kitu kilicho bora zaidi. “Nitawaundia wanawake hawa chombo chini ya ukuhani kwa mfano wa ukuhani,” alisema.4
Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama haukuwa kama kikundi kingine cha wanawake kikijaribu kufanya mema duniani. Ulikuwa tofauti. Ulikuwa ‘kitu bora zaidi’ kwa sababu uliundwa chini ya mamlaka ya ukuhani. Kuundwa kwake kulikuwa hatua muhimu katika mwanzo wa kazi ya Mungu ulimwenguni.5
Maandiko na Taarifa za Ziada
Mafundisho na Maagano 25:2–3, 10; 88:73; reliefsociety.lds.org
© 2017 na Intellectual Reserve, Inc. Haki zote zimehifadhiwa. Imepigwa chapa Marekani. Idhinisho la Kiingereza: 6/16. Idhinisho la kutafsiri: 6/16. Tafsiri ya Visiting Teaching Message, January 2017. Swahili. 97921 743