2017
Tayari Nilikuwa Nimeamua
March 2017


Vijana

Tayari Nilikuwa Nimeamua

Mwandishi anaishi Utah, Marekani.

Wakati mmoja nilipokea somo la thamani katika darasa la Wasichana kuhusu usafi wa kimwili—mada ambayo ilisababisha wengi wa vijana kufadhaika vitini mwao. Sikumbuki kila kitu nilichojifunza siku hiyo, lakini ninakumbuka kiongozi wangu akizungumzia mojawapo ya kiwango gezo chake binafsi ni kuwa—sikuzote kusalia msafi kimwili. Maneno yake yalibakia nami, na kisha nikafanya uamuzi wa makusudi wa kukiasili na kufanya kama mojawapo ya maadili yangu binafsi.

Siku mmoja nilipokuwa nikisafiri kwenda nyumbani nikiwa kwenye basi kutoka katika tukio la spoti, mtu fulani alianzisha mchezo wa kusema ukweli au kuthubutu. Tukiwa tumechoshwa, baadhi ya watoto na mimi tulijiunga. Ilipofikia wakati wangu, nilithubutiwa kutenda kitu ambacho nilijua hakikuwa sahihi. Huu ungelikuwa uamuzi mgumu kwangu kufanya, lakini maneno ya kiongozi wangu wa Wasichana yalinijia akilini, na uchaguzi ulikuwa rahisi. Mara moja nilikataa. Nilikuwa tayari nimekwisha amua kile ambacho ningefanya katika hali kama hiyo.

Ninajua ya kwamba wakati tunapoenda kanisani na kutengeneza nafasi ya mambo ambayo tunafundishwa huko, tutabarikiwa kwa uwezo mkubwa zaidi wa kiroho na ulinzi kutokana na majaribu ya ulimwengu.

Chapisha