2017
Nguvu Zinazowezesha za Yesu Kristo na Upatanisho Wake.
March 2017


Ujumbe wa Mwalimu Mtembeleaji, Machi 2017

Nguvu Zinazowezesha za Yesu Kristo na Upatanisho Wake.

Kwa maombi jifunze maneno haya na utafute maongozi kujua kitu cha kufundisha. Ni kwa namna gani kuelewa lengo la Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama kutawatayarisha mabinti wa Mungu kwa ajili ya baraka za uzima wa milele?

Picha
Relief Society seal

Imani, Familia, Usaidizi

“Nayaweza mambo yote katika yeye anitiaye nguvu” (Wafilipi 4:13). “Ingawaje sisi sote tuna udhaifu, tunaweza kuushinda,” alisema Rais Dieter F. Uchtdorf, Mshauri wa Pili katika Urais wa Kwanza. Kwa kweli ni kwa neema ya Mungu kwamba, kama tunajinyenyekeza wenyewe na kuwa na imani, vitu dhaifu vinaweza kuwa vya nguvu.”1

Mwokozi wetu anasema katika Mafundisho na Maagano, “Nitaenda mbele yako. Nitakuwa mkono wenu wa kuume na wa kushoto, na Roho wangu atakuwa mioyoni mwenu, na malaika zangu watawazingira, ili kuwabeba juu” (M&M 84:88).

“Nefi alikuwa mfano wa mtu ambaye alijua na kuelewa na kutegemea uwezo unaowezesha wa Mwokozi,” asema Mzee David A. Bednar wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili. “Ndugu zake Nefi walimfunga kwa kamba na kupanga kumuangamiza. Tafadhali angalia maombi ya Nefi: ‘Ewe Bwana, kulingana na imani yangu kwako, unikomboe kutoka mikononi mwa ndugu zangu; ndio, hata unipatie nguvu ili nizikate kamba ambazo nimefungwa nazo’ (1 Nefi 7:17; mkazo umeongezewa).

“… Nefi hakuomba ili hali yake ibadilishwe. Badala yake, aliomba apate nguvu za kubadilisha hali yake. Na ninaamini aliomba kwa njia hii hasa kwa sababu alijua, alielewa na kupata uzoefu wa uwezo wa kuwezesha wa Upatanisho.

“Siamini kwamba kamba ambazo Nefi alikuwa amefungwa nazo zilianguka kutoka mikononi mwake kimiujiza. Badala yake, ninashuku ya kwamba alibarikiwa na kuwa na kutokata tamaa na nguvu binafsi zilizokuwa zaidi ya uwezo wake, kiasi kwamba ‘kwa nguvu za Bwana’ (Mosia 9:17) alifanya kazi na kuzigeuza geuza na kuzivuta kwa nguvu zile kamba, na hatimaye na kwa ukweli aliwezeshwa kuzikata zile kamba.”2

Maandiko na Taarifa za Ziada

Isaya 41:10; Etheri 12:27; reliefsociety.lds.org

Muhtasari

  1. Dieter F. Uchtdorf, “Kipawa cha Neema,” Liahona, Mei 2015, 108.

  2. David A. Bednar, “Nguvu zaidi ya Yetu,” New Era, Machi. 2015, 4.

Chapisha