2017
Mmisionari asiye na Kibandiko cha jina
June 2017


Vijana

Mmisionari asiye na Kibandiko cha jina

Shuleni nina mwalimu ambaye ana tabia inayoweza kumwogopesha mtu kuchangia mawazo tofauti kuhusu kitu kinachojadiliwa. Siku moja tulikuwa tukizungumzia mada ya wamisionari wa Siku za Mwisho. Nilijua ningeliweza kujibu maswali yake, lakini nilihisi nisifanye hivyo. Hivyo basi nilizungumza kiasi tu cha kuweza kumridhisha wakati ule.

Kwa wiki chache zilizofuata sikuweza kuacha kufikiria kuhusu yale mazungumzo yetu. Hatimaye, wazo lilinijia kwamba nilipaswa kumpatia Kitabu cha Mormoni pamoja na kuweka alama mistari michache kuhusu kazi ya umisionari. Wazo liliniogopesha, lakini liliendelea kuwepo akilini mwangu. Nilijua lilikuwa ni ushawishi nililopaswa kuufuata.

Karibu miezi miwili baadae, nilikiweka tayari Kitabu cha Mormoni. Siku nzima nilihisi kama kitabu kinaunguza tundu katika begi langu la mgongoni. Sekunde tatu zilizonichukua mimi kukikabidhi kitabu hicho kwake wakati nikiondoka kwa ajili ya mapumziko ya majira ya baridi, kilikuwa ni kitu kilichoniogopesha sana katika maisha yangu.

Siku ya kwanza niliporudi, nilipita katika darasa lake lakini niliogopa kuingia. Halafu nikamsikia akiniita, na alinipatia kadi. Niliisoma nikiwa kwenye ushoroba. Aliandika kwamba amejifunza “kwa kiasi kikubwa” mistari niliyoitia alama, na alianza gundua baadhi ya sababu nyuma ya imani yangu.

Nimepata hamasa ya kushiriki injili sasa, na nimehamasika zaidi hata kumtumikia Baba yangu wa Mbinguni katika misheni hivi karibuni.

Chapisha