2017
Nguvu ya Ukuhani kupitia Kushika Maagano
June 2017


Ujumbe wa Ualimu wa kutembelea, Juni 2017

Nguvu ya Ukuhani kupitia Kushika Maagano

Kwa maombi jifunze nyenzo hii na utafute maongozi ili kujua kitu cha kushiriki. Ni kwa namna gani kuelewa lengo la Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama kutawatayarisha mabinti wa Mungu kwa ajili ya baraka za uzima wa milele?

Relief Society seal

Imani Familia Usaidizi

“Ujumbe wangu kwa … wote ni kwamba tunaweza kuishi kila saa ‘tukibarikiwa kwa uwezo wa nguvu za ukuhani,’ licha ya hali zetu,” Alinena Mzee Neil L. Andersen wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili.

“… Nashuhudia kwamba mnaposhiriki kwa ustahiki katika ibada za ukuhani, Bwana atawapeni nguvu kubwa, amani, na mtazamo wa milele. Bila kujali hali yako, nyumba yako itabarikiwa kwa nguvu za uwezo wa ukuhani.’”1

Tunawezaje kualika nguvu ya ukuhani katika maisha yetu? Mzee M. Russel Ballard wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili anatukumbusha kwamba “wale walioingia katika maji ya ubatizo na kisha kupokea endaumenti zao katika nyumba ya Bwana wanastahiki utajiri wa baraka za kufurahisha. Endaumenti kiuhalisia ni zawadi ya kuwa na nguvu … [na] Baba yetu wa Mbinguni ni mkarimu kwa nguvu Yake. Anatukumbusha kwamba wanaume na wanawake wanapoenda hekaluni, “wao hupewa nguvu sawa”, “ambayo kwa tafsiri ni nguvu ya ukuhani.”2

Linda K. Burton, Rais Mkuu wa Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama, alisema: “Kwa kuwa nguvu ya ukuhani ni kitu ambacho sote tunatamani kuwa nacho katika familia na nyumba zetu, ni kitu gani yatupasa, sisi kufanya ili kualika nguvu hiyo katika maisha yetu? Wema wa kibinafsi ni lazima ili kupata nguvu ya ukuhani.3

“Kama tutajiwasilisha wenyewe kwa unyenyekevu mbele za Bwana na kumwomba Yeye atufundishe, Yeye atatuonesha jinsi ya kuongeza ufikiaji wetu katika uwezo Wake,” alisema Rais Russell M. Nelson, Rais wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili.4

Maandiko na Maelezo ya Ziada

1 Nefi 14:14; Mafundisho na Maagano 121:36; 132:20; reliefsociety.lds.org

Muhtasari

  1. Neil L. Anderson, “Nguvu katika Ukuhani,” Liahona, Nov. 2013, 92, 95.

  2. M. Russell Ballard, “Wanaume na Wanawake na Nguvu ya Ukuhani,” Liahona, Sept. 2014, 36.

  3. Linda K. Burton, “Nguvu za Ukuhani—Zipo kwa Wote,” Liahona, Juni 2014, 21.

  4. Russell M. Nelson, “Gharama za Nguvu za Ukuhani,” Liahona, May 2016, 69.