Vijana
Wakati Rafiki Yangu Alipofariki
Mwandishi anaishi Utah, Marekani.
Wakati wa mwaka wangu wa kwanza katika Shule ya Sekondari, rafiki yangu alipatwa na ugonjwa wa neva kwenye ubongo na alifariki siku iliyofuata. Ingawa nilikuwa mshiriki wa Kanisa, bado nilihangaika. Nimefundishwa maisha yangu yote kwamba ninaweza kumgeukia Baba wa Mbinguni na Mwokozi kwa chochote, lakini kamwe sikuhitaji kwenda kupitia kitu kama hiki hapo mwanzo.
Nililia kwa masaa mengi, nikijaribu kutafuta kitu fulani—chochote—ili kinipe amani. Usiku baada ya kifo chake, niligeukia kitabu cha nyimbo. Nilipokuwa napekua kurasa, nilitua kwenye “Abide with Me; ’Tis Eventide,” (Wimbo, na. 165). Mstari wa tatu ulinigusa sana:
Kaa Nami ni Usiku Sana,
Usiku Utakuwa na Upweke
Kama Siwezi Kuongea Nawe,
Wala Kuona Nuru Yangu Kwako.
Giza la Ulimwengu, Naogopa,
Utakaa Nyumbani Mwangu
Ee Mwokozi, Kaa Nami Usiku Huu;
Tazama, ni Usiku Sana.
Mstari huu ulinijaza na amani tele. Nilijua wakati ule kwamba sio tu Mwokozi angeweza kukaa usiku ule pamoja nami bali kwamba pia Yeye alijua kwa usahihi jinsi nilivyokuwa najisikia. Najua kuwa upendo niliousikia kupitia wimbo ule sio tu uliniwezesha kupita usiku ule bali umeniwezesha kupita majaribu mengine mengi niliyostahimili.