2017
Ili Waweze Kuwa Wamoja
July 2017


Ujumbe wa Ualimu wa Kutembelea, Julai 2017

Ili Waweze Kuwa Wamoja

Kwa maombi jifunze maneno haya na utafute maongozi kujua kitu cha kufundisha. Ni kwa namna gani kuelewa madhumuni ya Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama kunawatayarisha mabinti wa Mungu kwa ajili ya baraka za uzima wa milele?

Picha
Relief Society seal

Imani Familia Usaidizi

“Yesu alijipatia umoja kamili na Baba kwa kujiweka mwenyewe, mwili na roho, katika mapenzi ya Baba,” alifundisha Mzee D. Todd Christofferson wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili

“… Hakika sisi hatuwezi kuwa wamoja na Mungu na Kristo hadi pale tutakapoyafanya mapenzi Yao na maslahi yao kuwa ndiyo hamu yetu kubwa. Unyenyekevu wa jinsi hiyo haufikiwi kwa siku moja, lakini kupitia kwa Roho Mtakatifu, Bwana atatufundisha kama tuko tayari mpaka, katika mchakato wa muda, inaweza kusemekana kwa usahihi zaidi kwamba Yu ndani yetu kama vile Baba alivyo ndani Yake.”1

Linda K. Burton, Rais Mkuu wa Muungano wa Usaidizi wa Akina Mama, alifundisha jinsi ya kufanya kazi kuelekea umoja huu: “Kufanya na kutii maagano yetu ni dhihirisho la msimamo wetu wa kutaka kuwa kama Mwokozi. Kilicho bora ni kujitahidi kwa ajili ya msimamo unaooneshwa vizuri ndani ya vifungu vichache vya maneno ya wimbo unaopendwa: “Nitakwenda Utakako niende. … Nitasema kile wewe, unataka mimi niseme. … Nitakuwa kile wewe unataka mimi niwe.”2,

Mzee Christofferson pia alitukumbusha kwamba “Tunapojitahidi siku baada ya siku na wiki baada ya wiki kufuata njia ya Kristo, roho yetu huthibitisha ufahari wake, vita ndani yetu inapungua, na majaribu yanakoma kutusumbua.”3

Neil F. Marriot, Mshauri wa Kwanza katika Urais Mkuu wa Wasichana, anatoa ushuhuda wa baraka za kujitahidi kuweka mapenzi yetu pamoja na mapenzi ya Mungu: “Nimepambana kuondoa hamu ya kibinadamu kufanya mambo kwa njia, yangu, hatimaye kutambua kwamba njia yangu ina mapungufu, ina kikomo, na ni duni ukilinganisha na njia ya Yesu Kristo. “[Njia ya Baba yetu wa Mbinguni] ni njia ambayo inaelekeza kwenye furaha katika maisha haya na uzima wa milele katika ulimwengu ujao.”4 Na tujitahidi kwa unyenyekevu kuwa wamoja pamoja na Baba yetu wa Mbinguni na Mwanae, Yesu Kristo.

Maandiko na Maelezo ya Ziada

Yohana 17:20–21; Waefeso 4:13; Mafundisho na Maagano 38:27–17; reliefsociety.lds.org

Muhtasari

  1. D. Todd Christofferson, “That They May Be One in Us,” Liahona, Nov. 2002, 72, 73.

  2. Linda K. Burton, “The Power, Joy, and Love of Covenant Keeping,” Liahona, Nov. 2013, 111.

  3. D. Todd Christofferson, “Ili waweze kuwa wamoja ndani yetu,” 71

  4. Neil F. Marriott, Yielding Our Hearts to God,` Liohona Nov.2015,32

Chapisha