Vijana
Kumkumbuka Bwana Kila Siku
Marafiki, majukumu ya nyumbani, kazi ya ziada, TV—kuna mambo mengi ambayo huhitaji usikivu wetu. Lakini kila wiki, tunamuahidi Baba wa Mbinguni “kwamba [sisi] daima tutamkumbuka [Mwanawe, Yesu Kristo]” (M&M 20:79).
Rais Eyring anasema ya kwamba tunaweza “kufanya chaguzi kila siku” ambazo zinatusaidia kumkumbuka Mwokozi. Zingatia kuweka lengo mwezi huu la kumkumbuka Mwokozi zaidi kila siku. Unaweza ukatengeneza ratiba na ukaahidi kufanya kitu kimoja kila siku ili kuimarisha uhusiano wako Naye. Rais Eyring anaorodhesha mambo kama vile kusoma maandiko, kusali kwa imani, na kumtumikia Mwokozi na wengine. Pia kuna kuandika shajara, kushiriki mikutano ya Kanisa, kusikiliza hotuba za mkutano mkuu, kwenda hekaluni, kuimba nyimbo za kidini—orodha inaendelea! Tunapomkumbuka Mwokozi kila siku, Rais Eyring anaahidi ya kwamba “Baraka … Zitakuja pole pole na kwa uhakika … [na] itatufanya kuwa wanafunzi wa kweli wa Bwana Yesu Kristo.