2017
Kuwa Tayari Kubebeana Mizigo
December 2017


Ujumbe wa Ualimu wa Kutembelea, Disemba 2017

Kuwa Tayari Kubebeana Mizigo

Kwa maombi jifunze nyenzo hii na utafute mwongozo wa kiungu ili kujua kitu cha kufundisha. Ni kwa namna gani kuelewa lengo la Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama kutawatayarisha mabinti wa Mungu kwa ajili ya baraka za uzima wa milele?

Imani Familia Usaidizi

“Tumezungukwa na wale wanaohitaji usikivu wetu, himizo letu, msaada wetu, faraja yetu, ukarimu wetu,” Rais Thomas S. Monson alisema. “Sisi ni mikono ya Bwana hapa duniani, tukiwa na jukumu la kuwatumikia na kuwainua watoto Wake. Anamtegemea kila mmoja wetu.”1

Rais Henry B. Eyring, Mshauri wa Kwanza katika Urais wa Kwanza, alisema: “Mabadiliko makuu yalianza ndani ya moyo wako wakati ulipoingia Kanisani. Uliweka agano, na ulipokea ahadi ambayo ilianza kubadilisha asili yako.

Uliahidi kwamba utamsaidia Bwana kuifanya mizigo ya [wengine] iwe miepesi na kuwafariji. Ulipewa uwezo wa kuwasaidia kupunguza uzito wa mizigo hiyo pale ulipopokea kipawa cha Roho Mtakatifu.”2

“Tunataka kutumia nuru ya injili kuwaona wengine kama Mwokozi anavyofanya—kwa huruma, tumaini, na upendo,” alisema Jean B. Bingham, Rais wa Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama. “Siku itakuja wakati tutakapokuwa na uelewa kamili wa mioyo ya wengine na tutakuwa na shukrani kuwa na huruma iliyoelekezwa kwetu—kama vile tunavyoelekeza mawazo na maneno ya upendo kwa wengine wakati wa maisha haya.

“Wajibu na fursa yetu ni kukumbatia maboresho katika kila mmoja tunapojitahidi kuwa zaidi kama Mwokozi wetu.”3

Tunapobebeana mizigo na kushika maagano yetu, tunafungua njia ambayo kwayo Yesu atawaponya wengine. Mzee Jeffrey R. Holland wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili alifundisha “Mkifikiria gharama isiyofikirika ya Kusulubiwa na Upatanisho, mimi nawaahidi Yeye hatatugeuzia mgongo Wake sasa. Anaposema kwa wale walio maskini katika roho, ‘Njooni kwangu,’ Yeye humaanisha Anajua njia ya kuponyokea na Yeye anajua njia ya kwenda juu. Yeye anaijua kwa sababu Ameshaipitia. Yeye anajua njia kwa sababu Yeye ndiye njia.”4

Maandiko ya Ziada

Mathayo 25:40; Wagalatia 6:2; Mosia 2:17; 18:8–9

Muhtasari

  1. Thomas S. Monson, “Serve the Lord with Love,” Liahona, Feb. 2014, 4.

  2. Henry B. Eyring, “The Comforter,” Liahona, May 2015, 18.

  3. Jean B. Bingham, “I Will Bring the Light of the Gospel into My Home,” Liahona, Nov. 2016, 6, 8.

  4. Jeffrey R. Holland, “Broken Things to Mend,” Liahona, May 2006, 71.