2021
Jinsi Gani Ninaweza Kujua Kwamba Ninasikia Sauti ya Bwana katika Maisha Yangu?
Februari 2021


“Jinsi Gani Ninaweza Kujua Kwamba Ninasikia Sauti ya Bwana katika Maisha Yangu?” Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana, Feb 2021, 29.

Ujumbe wa kila Mwezi wa Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana, Februari 2021

Jinsi Gani Ninaweza Kujua Kwamba Ninasikia Sauti ya Bwana katika Maisha Yangu?

Picha
kijana akisoma maandiko

Rais Russell M. Nelson ametualika “kufikiri kwa kina na mara kwa mara” kuhusu jinsi tunavyomsikia Yesu Kristo na “kuchukua hatua ili kumsikia vyema zaidi na mara kwa mara” (“‘Jinsi Gani Wewe #UnamsikiaYeye?’ Mwaliko Maalum,” Feb. 26, 2020, blog.ChurchofJesusChrist.org).

Tunaweza kumsikia kupitia maandiko na maneno ya manabii. Lakini sio tu kumsikia au kusoma maneno hayo ndiyo muhimu. Kupitia Nabii Joseph Smith, Bwana alieleza:

“Ni sauti yangu ambayo inasema [maneno haya] kwenu; kwani yametolewa na Roho yangu kwenu … ;

“Kwa hiyo basi, ninyi mnaweza kushuhudia kwamba mmesikia sauti yangu” (Mafundisho na Maagano 18:35–36).

Kwa nyongeza, kutafuta kumsikia Yeye sio kitu tunachofanya kwa kukurupuka. Rais Nelson, amesema “Inahitaji ufahamu na juhudi endelevu” (“Msikilize Yeye,” mkutano mkuu wa Aprili 2020 [Ensign au Liahona, Mei 2020, 89]).

Unapojifunza, unapoomba, unapoabudu, unapohudumu, na unapotii amri za Mungu, Yeye atakubariki na Roho Wake na kupitia Upatanisho wa Yesu Kristo, atakubadilisha. Ndipo utaweza kujua umesikia sauti Yake.

Chapisha