2021
Ziara ya Yohana Mbatizaji
Februari 2021


“Ziara ya Yohana Mbatizaji,” Rafiki, Februari 2021

Ujumbe wa kila mwezi wa gazeti la Rafiki, Februari 2021

Ziara ya Yohana Mbatizaji

Picha
Joseph Smith na Oliver Cowdery wakiomba

Vielelezo na Apryl Stott

Siku moja Joseph Smith na Oliver Cowdery walikuwa na swali. Je, ni njia ipi ilikuwa sahihi ya kubatizwa? Waliomba ili kujua jibu.

Picha
Yohana Mbatizaji

Malaika alikuja. Alikuwa Yohana Mbatizaji. Yule aliyembatiza Yesu. Aliwaambia kwamba walihitaji ukuhani ili kubatiza watu.

Picha
Yohana Mbatizaji akimpa Ukuhani wa Haruni Joseph Smith

Yohana aliwabariki Joseph na Oliver. Aliwapa ukuhani. Sasa wangeweza kubatiza watu katika jinsi Yesu alivyobatizwa.

Picha
Oliver Cowdery akimbatiza Joseph Smith

Joseph alimbatiza Oliver katika mto. Kisha Oliver akambatiza Joseph. Baadaye, wengine wengi walibatizwa pia.

Picha
baba akimbatiza binti yake

Kwa sababu Baba wa Mbinguni alijibu maombi ya Joseph Smith, ukuhani umerudi tena duniani! Ninaweza kubatizwa kama Yesu alivyobatizwa.

Ukurasa wa Kupaka Rangi

Tunaweza Kubatizwa

Picha
A pencil drawing of Joseph baptizing Oliver Cowdery.

Je, unaweza kufanya nini ili kumfuata Yesu Kristo?

Chapisha