2021
Mungu Alituambia Tubatizwe
Februari 2021


“Mungu Alituambia Tubatizwe,” Liahona, Februari 2021

Ujumbe wa kila mwezi wa gazeti la Liahona , Februari 2021

Mungu Alituambia Tubatizwe

Yesu Kristo aliweka mfano wa kubatizwa na mtu mwenye mamlaka ya Mungu.

Ingawa hatuna maelezo mengi kuhusu maisha binafsi ya Yesu Kristo, tunajua kwamba Yeye alibatizwa alipokuwa na umri karibia miaka 30 (ona Luka 3:23). Hivi ni baadhi ya vitu tunavyojifunza kuhusu ubatizo kutokana na mfano Wake.

Kwa Ajili ya Kila Mtu

Kama tuna umri wa kutosha na tumekua vya kutosha kuelezea tofauti kati ya jema na baya, Baba wa Mbinguni anatutaka sisi tubatizwe (ona Mafundisho na Maagano 18:42). Yesu alikuwa mkamilifu, lakini bado alichagua kubatizwa ili kufuata amri za Mungu (ona Mathayo 3:13–17; 2 Nefi 31:7). Hata wale ambao wamekwisha kufa wanaweza kuukubali ubatizo. Tunautoa kwao kwa kubatizwa kwa niaba yao katika mahekalu. (Ona Mafundisho na Maagano 128:15–18.)

Picha
ubatizo

Unafanywa kwa Mamlaka

Yesu hakubatizwa tu na mtu yeyote yule. Yeye mahususi alikwenda kwa binamu Yake Yohana, aliyekuwa na mamlaka ya ukuhani kutoka kwa Mungu. Baada ya Yesu kufa na wanafunzi Wake kuuawa, mamlaka hayo ya ukuhani yalipotea duniani. Kisha, mnamo mwaka 1829, Yohana Mbatizaji alimtokea Joseph Smith na alimpa mamlaka ya kubatiza katika jina la Mungu. Kwa sababu ya Urejesho huo, tunaweza kubatizwa na mamlaka yale yale leo.

Picha
urejesho wa Ukuhani wa Haruni

Ahadi ya Pande Mbili

Ubatizo unajumuisha ahadi ya pande mbili, au agano, kati yetu sisi na Mungu. Sisi tunaahidi:

  1. Kujichukulia juu yetu jina la Kristo.

  2. Daima kumkumbuka Yeye.

  3. Kutii amri Zake.

Kwetu sisi, Mungu anaahidi kwamba Roho Wake daima atakuwa pamoja nasi. Maneno ya sala za sakramenti hutukumbusha juu ya agano hili kila wiki. (Ona Mafundisho na Maagano 20:77, 79.)

Picha
familia ikiwa katika mkutano wa sakramenti

Kumpokea Roho Mtakatifu ni Sehemu Muhimu ya Ubatizo

Baada ya Yesu kubatizwa, Roho Mtakatifu alitokea katika umbile la njiwa (ona 2 Nefi 31:8). Leo, baada ya watu kubatizwa, wanathibitishwa. Hii inamaanisha wanapokea baraka maalumu ambamo ndani yake wao hualikwa kupokea kipawa cha kiroho cha utakaso cha Roho Mtakatifu (ona 2 Nefi 31:17). Roho Mtakatifu anaweza kutuonya sisi juu ya hatari, kutufariji, kutuongoza ili kufanya maamuzi mazuri, na kutusaidia kuhisi upendo wa Mungu (ona Mafundisho na Maagano 39:6).

Picha
mwanamke akithibitishwa

Tunaweza Kutubu Daima

Mungu alijua kwamba tutafanya makosa. Licha ya jitihada zetu bora, tungetenda dhambi na kushindwa kuishi kulingana na ahadi zetu za ubatizo. Kwa hiyo anatupa kila mmoja wetu nafasi ya kutubu. (Ona Mafundisho na Maagano 18:13.) Kila siku tunaweza kujitahidi kwa uwezo wetu wote ili kuomba msamaha na kusahihisha makosa yoyote. Tunaweza kusali na kumwomba Mungu msamaha. Ndipo, tunaposhiriki sakramenti kwa moyo wa unyenyekevu, Roho Mtakatifu anaweza kuwa pamoja na sisi (ona 3 Nefi 18:11).

Picha
mwanamke akiomba pembeni ya kitanda

Maandiko Yanasema Nini kuhusu Ubatizo?

Wazazi wanapaswa kuwasaidia watoto wao kujiandaa kwa ajili ya ubatizo (ona Mafundisho na Maagano 68:25).

Wale walio chini ya umri wa miaka minane hawahitaji kubatizwa (ona Moroni 8).

Wakati tunapobatizwa, tunaahidi “kuomboleza na wale wanaoomboleza; … kuwafariji wale ambao wanahitaji kufarijiwa, na kusimama kama mashahidi wa Mungu nyakati zote na katika vitu vyote, na katika mahali popote” (Mosia 18:9).

Chapisha