“Wamisionari Walihubiri Injili,” Rafiki, Aprili 2021
Ujumbe wa kila mwezi wa gazeti la Rafiki, Aprili 2021
Wamisionari Walihubiri Injili
Baada ya Kitabu cha Mormoni kupigwa chapa, Mungu aliwaita wamisionari waende kuwafundisha watu zaidi kuhusu kitabu hicho.
Kaka wa Joseph Smith, Samuel, alibeba begi lililojaa nakala za Kitabu cha Mormoni kwa ajili ya kuzigawa. Watu walikusanyika ili kumsikiliza akifundisha.
Wamisionari wengine walifundisha watu huko Ulaya. Wengine walifundisha watu waliokuwa wakiishi katika visiwa.
Baadaye, akina dada wamisionari rasmi wa kwanza waliitwa kuhudumu huko Uingereza.
Ninaweza kuwa mmisionari pia. Ninaweza kushiriki Kitabu cha Mormoni na wengine.
© 2021 na Intellectual Reserve, Inc. Haki zote zimehifadhiwa. Imepigwa chapa Marekani. Idhini ya Kiingereza: 6/19. Idhini ya kutafsiri: 6/19. Tafsiri ya Monthly Friend Message, April 2021. Swahili. 17467 743