2022
Ruthu na Naomi
Juni 2022


“Ruthu na Naomi,” Jumbe za kila mwezi za gazeti la Rafiki, Juni 2022

“Ruthu na Naomi”

Jumbe za kila mwezi za gazeti la Rafiki Juni 2022

Ruthu na Naomi

Picha
Ruthu kuolewa na familia ya Naomi

Vielelezo na Apryl Stott

Naomi na familia yake walikwenda kwenye nchi mpya kwa sababu ya njaa. Walikutana na binti aliyeitwa Ruthu. Ruthu aliolewa na mwana wa Naomi.

Picha
Ruthu na mume anayeaga dunia

Kisha mume wa Ruthu alifariki. Ruthu alikuwa na huzuni sana.

Picha
Naomi

Naomi naye alihuzunika sana. Hakuwa amebaki na familia ya kumtunza. Naomi aliamua kurejea katika nchi aliyotoka.

Picha
Naomi na Ruthu

Naomi akamwambia Ruthu arejee kwa familia yake. Lakini Ruthu alimpenda Naomi. Aliahidi kuambatana na Naomi na kumtunza.

Picha
Ruthu akikusanya

Ruthu na Naomi walikuwa maskini. Kwa hiyo Ruthu alifanya kazi kwa bidii ili kutafuta chakula.

Picha
Boazi na Ruthu wakiwa shambani

Siku moja mwanaume anayeitwa Boazi alimwona Ruthu akikusanya mabaki ya nafaka katika moja ya shamba lake.

Picha
Boazi pamoja na mtumishi

Boazi alikuwa mwema. Aliwaambia wafanyakazi wake wamuachie Ruthu chakula cha ziada.

Picha
Ruthu, Boazi na Naomi, pamoja na mtoto

Baadaye Ruthu na Boazi walioana. Walipata mtoto wa kiume. Naomi alisaidia kwenye kumtunza.

Picha
familia ikipakua chakula

Ninaweza kusaidia kuwatunza wengine. Ninaweza kuwa mkarimu kwa wenye uhitaji.

Ukurasa wa Kupaka Rangi

Ninaweza Kuwajali Wengine

Picha
watoto wakiwa na babu

Bonyeza kwenye picha ili kupakua.

Kielelezo na Apryl Stott

Je, unaweza kumsaidia nani?

Chapisha