2022
Je, Ni Nini Hutendeka katika Mikutano ya Kanisani ya Jumapili?
Juni 2022


“Je, Ni Nini Hutendeka katika Mikutano ya Kanisani ya Jumapili?,” Liahona, Juni 2022.

Ujumbe wa kila mwezi wa gazeti la Liahona , Juni 2022

Je, Ni Nini Hutendeka katika Mikutano ya Kanisani ya Jumapili?

Wanawake wawili wakikumbatiana

Waumini wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho hukusanyika kila Jumapili kumwabudu Mungu na kufundishana injili ya Yesu Kristo. Wote wanakaribishwa kuhudhuria na waumini watapata nafasi ya kusali, kuhubiri na kufunza masomo kama wanataka. Mikutano hii huwasaidia waumini kuimarishana katika imani na “kuiunganisha mioyo yao kwa umoja na upendo” (Mosia 18:21).

mvulana katika kiti cha magurudumu akipitisha sakramenti

Mkutano wa Sakramenti

Waumini wa kata au tawi hukusanyika kila Jumapili kwa ajili ya mkutano wa sakramenti. (Wale wasio wa imani yetu wanakaribishwa kuhudhuria pia.) Sakramenti hutolewa kwa waumini wakati wa mkutano huu ili kuwasaidia wao kumkumbuka Yesu Kristo (ona makala ya Mambo ya Msingi ya Injili ya Aprili 2022 kwa maelezo zaidi kuhusu sakramenti). Mkutano pia unajumuisha sala, muziki wa kuabudu na mazungumzo yanayotolewa na waumini kuhusu injili ya Yesu Kristo.

wasichana wawili wakitabasamu kanisani

Mikutano Mingine

Baada ya mkutano wa sakramenti, waumini huelekea kwenye madarasa na akidi. Watoto wa umri wa miezi 18 hadi miaka 11 huudhuria Msingi. Jumapili ya kwanza na ya tatu za kila mwezi, waumini wengine wote wanahudhuria Shule ya Jumapili. Jumapili ya pili na ya nne, wanahudhuria mikutano ya Muungano wa Usaidizi, Wasichana au ya akidi ya ukuhani.

Sala

Sala katika mikutano ya Kanisa hutolea na waumini. Sala ni rahisi na hufuata mwongozo wa Roho Mtakatifu. Waumini huomba wakitumia maneno yanayoonyesha upendo na heshima kwa Baba wa Mbinguni. Hii ni pamoja na kutumia viwakilishi Wewe, Yako, na Wako wakati wa kumwomba Yeye.

Mahubiri

Mshiriki wa uraisi wa uaskofu au tawi huwaomba waumini kutoa mahubiri katika mkutano wa sakramenti. Mahubiri haya yanafokasi kwenye injili ya Yesu Kristo. Wanenaji wanatumia maandiko matakatifu na maneno ya viongozi wa Kanisa pale wanapoandaa mahubiri yao. Pia wanatoa ushuhuda wa baraka za kanuni za injili katika maisha yao.

Masomo

Baada ya mkutano wa sakramenti, waumini wanajifunza kuhusu injili katika madarasa ya watu wachache. Masomo haya yanawezakuwa kuhusu maandiko, mafundisho kutoka kwenye mkutano mkuu au mada nyingine. Hata kama mwalimu ataongoza somo, haimaanishi ni mhadhara. Waumini wote wa darasa wanaweza kutoa maoni yao kuhusu mada.

mtu akiongea kwenye mimbari kanisani

Ushuhuda

Mkutano wa sakramenti unajumuisha mkutano wa ushuhuda mara moja kwa mwezi. Kwa kawaida hii hufanyika Jumapili ya kwanza ya mwezi. Wakati wa mkutano huu, waumini wanaweza kutoa shuhuda zao kuhusu Yesu Kristo na injili Yake. Kutoa ushuhuda kunamaanisha kutangaza kweli za injili kama iliyofunuliwa na Roho Mtakatifu.

Matayarisho

Waumini wanajitayarisha kwa mikutano ya Jumapili kwa kuomba, kusoma maandiko na kuwa tayari kupokea ufunuo kutoka kwa Roho Mtakatifu. Ukiombwa kutoa hubiri au kufundisha somo, kwa sala fikiria kuhusu jinsi unavyoweza kufunza kanuni za injili. Kutumia maandiko. Toa ushuhuda wa kweli. Viongozi wako wa Kanisa wanaweza kukusaidia kujitayarisha, kama itahitajika.