2023
Je, Tunahitaji Kuwa Wakamilifu Sasa?
Februari 2023


“Je, Tunahitaji Kuwa Wakamilifu Sasa?” Kwa Ajili ya Nguvu Kwa Vijana, Februari 2023

Ujumbe wa kila mwezi wa Kwa ajili ya Nguvu kwa Vijana, Februari 2023

Je, Tunahitaji Kuwa Wakamilifu Sasa?

Picha
mvulana akisoma maandiko

Vielelezo na Emily E. Jones

Maandiko yaliandikwa ili kutubariki na kutuhimiza sisi, na hakika yanafanya hivyo. Lakini umetambua kwamba kila wakati kifungu cha maneno hujitokeza ambacho kinatukumbusha kwamba sisi tuna mapungufu? Kwa mfano: “Mtakuwa wakamilifu, kama Baba yenu … aliye mbinguni alivyo mkamilifu” (Mathayo 5:48). Kwa amri hiyo, tunataka kurudi kitandani na tujifunike hadi kichwani. Lengo kama hili la kiselestia linaonekana kutushinda. Lakini hakika Bwana hawezi kutupatia amri Anayojua kwamba tutashindwa kuitii.

Picha
msichana akiwa na mwamvuli katika mvua

“Ndio, mje kwa Kristo na mkamilishwe ndani yake,” Moroni anaomba. “Mpende Mungu na mioyo yenu, akili na nguvu zenu zote, kwamba … kwa neema yake mngekamilika katika Kristo” (Moroni 10:32; msisitizo umeongezwa). Tumaini letu pekee kwa ukamilifu wa kweli ni kupokea hilo kama zawadi kutoka mbinguni—hatuwezi “kununua”.

Picha
msichana akipanda juu kilimani na mbwa

Isipokuwa kwa Yesu, hakujakuwa na utendaji usio na kasoro katika safari hii ya kidunia tunayopita, hivyo tukiwa hapa duniani acheni tujitahidi kwa jitihada endelevu na kuepuka matarajio ya kupita kiasi juu yetu sisi wenyewe na juu ya wengine.

Picha
merikebu kwenye bahari yenye tufani

Kama tutastahimili, basi mahali fulani katika umilele utakaso wetu utamalizika na kuwa kamili—ambao ndiyo maana ya Agano Jipya ya ukamilifu.

Chapisha