“Kutumia Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Akidi za Ukuhani wa Haruni na Madarasa ya Wasichana,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Akidi za Ukuhani wa Haruni na Madarasa ya Wasichana: Mada za Mafundisho 2021 (2020)
“Kutumia Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Akidi za Ukuhani wa Haruni na Madarsaa ya Wasichana,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Akidi za Ukuhani wa Haruni na Madarasa ya Wasichana: Mada za Mafundisho 2021
Kutumia Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Akidi za Ukuhani wa Haruni na Madarasa ya Wasichana
Ni yapi madhumuni ya mikutano ya akidi na madarasa yetu?
Bwana amekuamini: Amekuita kutumikia katika urais wa akidi ya Ukuhani wa Haruni au urais wa darasa la Wasichana. Sehemu ya jukumu lako ni kuongoza na kusimamia mikutano ya Jumapili ya akidi au darasa lako. Kufanya hivi, husaidia kuelewa kwa nini tuna mikutano hii.
Mikutano ya akidi ya Ukuhani wa Haruni na darasa la Wasichana ni tofauti na madarasa mengineyo ya Kanisani kama vile Shule ya Jumapili na seminari. Katika mkutano wa akidi au darasa, tunafanya zaidi ya kujifunza mada ya injili. Tunajifunza kuhusu kazi ambayo Mungu ametupatia, na tunawapanga washiriki wa akidi au darasa letu kufanya kazi hiyo katika nyumba zetu, Kanisani, na katika jamii yetu. Tunapanga, kwa mfano, jinsi tutakavyotimiza majukumu yetu kama sehemu ya jeshi la vijana la Bwana kusaidia kuikusanya Israeli. Katika mikutano hii, hatuzungumzii tu kuhusu kazi—tunaweka mipango ya kuifanya.
Lakini msisitizo huu kwenye kazi haumaanishi kwamba tunaacha majadiliano ya mafundisho kwa ajili ya Shule ya Jumapili pekee. Kwa kweli, kujifunza mafundisho katika mikutano ya akidi na ya Wasichana ni muhimu—hutusaidia kuelewa sababu ya kwa nini tunafanya kazi. Tunapojifunza injili kwa pamoja, kweli tunazojifunza zinaweza kubadili mioyo yetu. Tunaweza kupokea misukumo kuhusu njia za kuongezeka “katika hekima na kimo, na katika kumpendeza Mungu na wanadamu” (Luka 2:52). Tunapokuwa tumeongoka zaidi katika Yesu Kristo na injili Yake, tutahisi hamu ya kusaidia wengine katika njia ya agano, ikijumuisha familia zetu, marafiki zetu, na washiriki wenzetu wa akidi na darasa.
Ni nani huongoza mikutano hii?
Mungu amewaita kama urais wa akidi na wa darasa na kuwapa mamlaka ya kuongoza. Hii ndio sababu kila mkutano wenu wa akidi au darasa lazima uongozwe na mshiriki wa urais wa akidi au darasa lako. Viongozi watu wazima hawana budi kutoa mwongozo na usaidizi, lakini hawatakiwi kuchukua majukumu yako. Ona sehemu yenye kichwa cha habari “Shaurianeni kwa Pamoja” mwanzoni mwa kila muhtasari katika nyenzo hii kwa ajili ya mawazo ya kukusaidia kujua jinsi ya kuongoza mkutano na kukamilisha lengo lake lililokusudiwa. Tumia mikutano ya urais kupanga jinsi utakavyoendesha mikutano hii ya Jumapili.
Je, ni nani atafundisha somo?
Viongozi watu wazima, mshiriki wa urais wa akidi au wa darasa, au mshiriki mwingine yeyote wa akidi au darasa anaweza kufundisha somo. Kama urais wa akidi au darasa, jadilianeni na viongozi wenu watu wazima kuhusu nani anatakiwa kupewa jukumu la kufundisha masomo. Kumbuka kwamba viongozi wenu watu wazima wana mengi ya kutoa. Tafuta kujifunza kutoka kwenye uzoefu na shuhuda zao. Pia kuna faida katika kuwaomba vijana kufundisha—kufundisha kunaweza kufanya uongofu wao kuwa wa kina na kujenga mahusiano imara na washiriki wengine wa akidi au darasa. Kwa hivyo wape fursa zinazofaa kufundisha somo lote au sehemu ya somo, lakini tilia maanani mahitaji na uwezo wa watu katika akidi au darasa lako. Kwa mfano, viongozi watu wazima wanaweza kufundisha mara nyingi kwenye akidi au madarasa pamoja na vijana wadogo au pamoja na vijana wenye uzoefu kidogo katika kufundisha injili. Wakati vijana wanapoalikwa kufundisha, mzazi au mtu mzima ambae ni mshauri hana budi kuwasaidia kujiandaa kadiri iwezekanavyo.
Wale waliopewa jukumu la kufundisha wanaweza kutumia sehemu yenye kichwa cha habari “Fundisha Mafundisho” katika kila muhtasari kwenye nyenzo hii katika kuwasaidia kujiandaa. Sehemu hii ina mapendekezo kwa ajili ya kufundisha na kujadili mafundisho ya wiki hiyo, lakini walimu hawatakiwi kuhisi kufungwa kwenye mapendekezo haya pekee. Kadiri Roho aongozavyo, walimu wanaweza kutohoa mawazo haya au kutumia ya kwao wenyewe kufundisha katika njia ambayo itatimiza mahitaji vizuri zaidi ya washiriki wa akidi au darasa na kuwasaidia kuelewa mafundisho.
Je, tutajadili mada zipi za mafundisho katika mikutano yetu?
Mada ya muhtasari wa kila wiki ni kanuni ya kimafundisho ambayo imechaguliwa kuendana na usomaji wa Mafundisho na Maagano uliopendekezwa kwa ajili ya wiki hiyo, ipatikanayo katika Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia. Kwa njia hii, majadiliano ya mafundisho katika mikutano ya akidi na darasa yataunga mkono kile vijana wanachojifunza nyumbani.
Japokuwa mihutasari itatakiwa kufundishwa katika Jumapili maalumu, bado unaweza kuwa na chaguo la kujadili mada zingine za mafundisho kulingana na mahitaji ya akidi yako au darasa lako.
Nyenzo hii inajumuisha mihutasari kwa ajili ya kila wiki wakati mikutano ya akidi ya Ukuhani wa Haruni na madarasa ya Wasichana inapofanyika. Mara kadhaa, unaweza kuhitaji kuruka somo kwa sababu ya mikutano ya kigingi au sababu zingine.
Je, ni nini jukumu la viongozi wetu watu wazima?
Viongozi wako watu wazima wana jukumu muhimu katika akidi za Ukuhani wa Haruni na madarasa ya Wasichana. Watakuongoza na kukushauri katika miito yako ya uongozi. Watakusaidia na kukuhimiza wakati unapofanya kazi ya akidi au darasa lako. Watakufundisha mafundisho, na watakuwa baraka kwako kupitia mfano wao, uzoefu, na ushuhuda.